Mambo Matatu(3) Muhimu Ya Kukufikisha Kwenye Mafanikio Makubwa, Ambayo Yanaanzia Kwenye Akili Yako.

Tumekuwa tunaandika na kukushirikisha makala nyingi sana kuhusu mafanikio.
Mpaka sasa umeshajifunza mbinu nyingi mno kuhusu mafanikio.
Kuanzia kuweka juhudi na maarifa kwenye kazi, kuwa mwaminifu, kuwa na matumizi mazuri ya muda wako, kuwa na mtizamo chanya, kuwa mvumilivu, kuwa na malengo na kuyafanyia kazi na mengine mengi muhimu sana.
Haya ni mambo muhimu sana ili kufikia mafanikio. Na yeyote anayeyafanya maisha yake hayawezi kuendelea vile ambavyo yapo sasa.

MFANO WA CHETI UTAKACHOPATA KWA KUSHIRIKI SEMINA YA MIMI NI MASHINDI, KUJIUNGA NA SEMINA HII BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Lakini mbinu zote hizi kuna watu wengi wanaozitumia, na katika watu hao kuna wachache wanafanikiwa na wengine wanashindwa kufanikiwa. Swali linakuja tatizo ni nini hapa? Kama wote wanatumia mbinu ile ile kwa nini wasifanikiwe sawa? Au kuna mambo ya bahati yanahusika hapo?

 

Moja ya vitu unavyoweza kuelezea kwenye hali kama hiyo ni tofauti ya uwezo kati ya watu, lakini hii bado ni sababu ya juu sana.
Leo kupitia makala hii utaijua ile sababu ya kweli kabisa ambayo inawatofautisha wanaoshinda na wanaoshindwa hata kama wote wanatumia mbinu sawa.
Kabla hatujaenda kwenye jambo hilo muhimu, sio vibaya kama tutajikumbusha misingi muhimu sana ya maisha.
 
Wanafalsafa wote na dini zote duniani zinakubaliana kwenye kitu kimoja kikubwa sana kuhusu maisha ya mtu. Kitu hiko ni kwamba kila unachofikiria kwa muda mrefu ndio kinachotokea kwenye maisha yako. Yaani kile ambacho unaruhusu kikae kwenye mawazo yako kwa muda mrefu ndio kinachotokea kwenye maisha yako.
Kwa njia hii basi, mtu ambaye ni mshindi na mwenye mafanikio anafikiri kuhusu ushindi na mafanikio kwa muda mrefu. Na mtu ambaye anashindwa kwenye kila jambo, huwa anafikiria kwa muda mrefu.
Akili yetu ina nguvu kubwa sana, ina nguvu ya kutumia yale mawazo tunayoyafikiria kwa muda mrefu na kuhakikisha inavutia yale mazingira yanayoendana na kile unachofikiria. Ndio maana kama unafanya kitu huku ukifikiria kushindwa tu ni nini kinatokea? Akili yako inahakikisha inakuletea mazingira yote ya kushinda.
Sasa tukirudi kwenye mfano wetu wa watu wawili ambao wanaweka juhudi sawa, mmoja anashinda mwingine anashindwa, ni kwamba anayeshinda anakuwa anafikiria kushinda muda mwingi na anayeshindwa huwa anafikiria kushindwa mara nyingi.
 
Mchezo hauishii hapo kwenye kufikiria tu, unakwenda mbali zaidi. Wanaoshinda hawafikirii tu kushinda, bali wanajiona kabisa wakishinda. Wanamichezo wengi walioshinda medali wanapohojiwa husema kile kilichotokea walikuwa wanakiona kila siku wakati wanafanya mazoezi. Yaani wanakuwa wamejijengea picha ya jinsi wanavyoshinda, jinsi watu wanavyowashangilia na wanaipitisha picha hii kwenye mawazo yao kila siku. Kwa ujanja na utii wa akili, inatengeneza mazingira yote kuhakikisha kwamba picha hii inajitokeza kweli.
Kufikiria kushinda, kupata taswira ya kushinda, sio hayo tu, washindi pia wanajinenea kauli za kushinda. Wanasema kwa sauti kabisa maneno yanayoashiria ushindi na hivyo akili yao inazama moja kwa moja kwenye ushindi.
Sasa walinganishe watu hawa wawili, mmoja anafikiria kushinda wakati wote, kila siku anakaa na kuiona taswira ya yeye akishinda kwenye akili yake, na pia anakaa na kujinenea maneno ya ushindi.
Mtu wa pili anafikiria kushindwa wakati wote, akikaa anapata taswira kabisa ya kushindwa na kila wakati anajinenea maneno ya kushindwa.
Na nipe jibu unafikiri ni yupi kati ya hao wawili atashinda? Nafikiri jibu unalo.
 
Unaondoka na nini hapa?
Vitu vitatu muhimu vya kuanza kufanya,
1. Kufikiria kushinda/kufanikiwa wakati wote(positive thinking)
2. Kujitengenezea taswira ya ushindi(visualization)
3. Kujinenea maneno ya ushindi(affirmation)
Lakini subiri, ni hivyo tu, na ninaanzaje kufanya mambo hayo?
Swali zuri sana na hapa ndio ninataka kukupa siri kubwa ambayo hujawahi kujifunza popote na wala hujawahi kuitumia.
Hapa nakushirikisha ujiunge na semina; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu. Semina hii imeandaliwa kwa misingi hiyo mitatu ambayo ni lazima itakufikisha kwenye ushindi na mafanikio.
Kwa kupata mafunzo ya semina utafikiri kuhusu mafanikio kwa muda mrefu na hii itakusogeza karibu na mafanikio.
Pia baada ya semina hii utapata cheti cha kukuonesha kwamba wewe ni msindi.
Hapa kwenye cheti ndio pazuri zaidi kwa sababu kunakamilisha sehemu ya pili na ya tatu.
Kwa cheti utakachokipata, (ona mfano kwenye picha hapo juu), utakuwa unakitumia kila siku kujiambia maneno ya mafanikio na kujenga taswira ya wewe kufanikiwa. Cheti hiki utakiweka mahali ambapo kila siku unapoamka au unapokuwa kwenye kazi yako unaweza kukisoma. Na utasoma maneno ya ushindi yaliyopo kwenye cheti hiko huku ukijijengea taswira ya wewe kushinda.
Kwa kufanya hivyo kila siku, pamoja na kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya, naweza kukuhakikishia kwamba hutabaki kama ulivyo sasa.
Je unataka kuipata nafasi hii ya kipekee ya kuweza kufikia ushindi na mafanikio?
Basi jiunge na semina hii itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao, ambapo utatumiwa email, utakuwa kwenye kundi la wasap na utatumiwa ujumbe mfupi kila siku kwa mwezi mmoja ukitengeneza kuwa mshindi.
Gharama za kushiriki semina hii ni tsh elfu 30, na mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii tarehe 02/10/2015, semina itaanza jumatatu tarehe 05/10/2015. Kama unataka kupata nafasi hii ya kipekee hakikisha unajiunga na semina hii leo hii, kwa KUBONYEZA MAANDISHI HAYA NA KUWEKA TAARIFA ZAKO na kisha kufanya malipo ya semina, tsh elfu 30(30,000/=) kwa namba hizi za simu; TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717396253 AU MPESA 0755953887. 
 
Kama hukupata taarifa ya awali ya mambo yatakayofundishwa kwenye semina hii ni haya hapa;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.

Kila siku utapokea somo moja ambalo litakujenga sana wewe kama mshindi. Na masomo yote yameandaliwa kama ahadi yako mwenyewe kwa nafsi yako. hii itabadili sana fikra zako na kuweza kujijengea taswira ya ushindi pamoja na kujinenea maneno ya ushindi.
Bado mpaka sasa hujajiunga? Bonyeza maandishi haya na uweke taarifa zako na kisha ufanye malipo ili kuhakikisha hukosi nafasi hii nzuri ya kubadili maisha yako.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: