Sababu Kubwa Zinazokufanya Ushindwe Kubadili Tabia Zinazokuzuia Kufikia Mafanikio Makubwa.

Wengi mara nyingi hutamani kubadili tabia mbaya walizonazo na kujijengea tabia bora za mafanikio, lakini kwa bahati mbaya hushindwa kufanya hivyo. Utakuta mtu anatamnai kuacha kuvuta sigara au tabia fulani mbaya lakini kila akijaribu anakuwa anashindwa kubadili tabia hiyo husika. Ni kitu ambacho kinawasumbua wengi akili na kushindwa kuelewa wafanye nini?
Je, ni mara ngapi umeshawahi kukutana na hali kama hii katika maisha yako ya kutaka kubadili tabia zako mbaya, halafu inakuwa inashindikana? Na umeshawahi kujiuliza ni kwa nini inakuwa ngumu kwako na kwa wengine kuweza kumudu kubadili tabia hizi na kujijengea tabia za mafanikio? Inawezekana ukawa unajua au hujui nini kinachosababisha.
Zifutazo Ni Sababu Kubwa Zinazokufanya Ushindwe Kubadili Tabia Zinazokuzuia Kufikia Mafanikio Makubwa.
1. Huanzi na mabadiliko madogo.
Kosa kubwa unalolifanya wakati unataka kubadili tabia zinazokuzuia kufanikiwa ni kutaka kwako wewe kuanza na mabadiliko makubwa. Hili ndilo kosa unalolifanya sana na kwa kosa hili unajikuta hakuna unachoweza kukibadili. Ili uweze kubadili tabia zako ni lazima uanze na mabadiliko madogo ambayo utayamudu.
Inawezekana kweli ukawa katika wakati mgumu kwa kuteswa na tabia fulani hilo sawa, lakini kumbuka huwezi kubadili tabia zako ghafla. Kama una tabia ya ulevi, ni vyema ukaanza kuiacha taratibu. Kama unataka kujenga tabia ya kuamka asubuhi na mapema pia ni vizuri ukaanza kwa kuamka hata dakika kumi kabla ya muda wa kawaida uliojiwekea. Hilo litakusaidia kufanikiwa kujenga tabia yoyote.
ANZA NA MABADILIKO KIDOGO KWANZA.
2. Unazuiliwa na  mazingira yanayokuzunguka.
Mara nyingi ili uweze kubadili tabia inayokusumbua, unashauriwa mara moja kubadili mazingira yanakufanya uendelee kuwa na tabia hiyo. Haiwezekani ukawa una mawazo chanya wakati katika maisha yako umezungukwa na watu wengi hasi, haiwezekani pia ukaachana na tabia ya ulevi wakati marafiki zako wengi ulionao wanatumia kilevi.
Ni lazima kubadili mazingira yako ili kufanikiwa kubadili tabia zako. Ikiwa hutaweza kubadili mazingira yanayokuzunguka tambua kwamba hutaweza kubadili chochote. Kwa hiyo, elewa mazingira uliyopo na kisha chukua jukumu la kuyabadili mara moja. Tofauti na hapo utasumbuka sana kubadili tabia zako na itabaki vilevile.
3. Unadharau mabadiliko madogo.
Siki zote mabadiliko ni mabadiliko hata yawe madogo vipi. Jijengee nia ya kubadilisha tabia zako mbaya na kujijengea tabia za mafanikio kila siku katika maisha yako hata kama ni kwa asilimia moja. Utakuwa tayari umefanya mabadiliko. Wengi sasa wanajikuta wanaendelea kubaki na tabia zao mbaya zinazowarudisha nyuma kwa sababu ya kudharau mabadiliko haya.
Kama kuna kitu unataka kukibadii hata kiwe kidogo vipi wewe chukua hatua ya kuelekea kwenye kukibadili. Acha kusimama na kusubiri mabadiliko makubwa sanasana utkuwa unajichelewesha wewe mwenyewa. Anzia pale ulipo a kidogo ulichonacho na endelea kusonga mbele. Hapo utakuwa umefanya uamuzi sahihi wa kubadili tabia zako na maisha kwa ujumla.
4. Hujajiwekea mipango imara.
Hapa mara nyingi kinachokuwa kinakuzuia kubadili tabia zako ni kutokuwa na utekelezaji wenye mwendelezo sahihi.  Kwa mfano Utakuta kesho umepanga kuamka asubuhi na mapema, ni kweli unafanya hivyo lakini baada ya siku mbili tatu unaacha kufanya hivyo. Kwa mtindo kama huo inakuwa ni ngumu kubadili tabia zako kwa sababu ya kukosa kujiwekea mipango imara ya kubadili tabia zako.
AMKA MTANZANIA inakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

Blog; www.dirayamafanikio.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: