Hakuna kati kati kwenye hilo,
Ni iwe inasaidia au la inaumiza.
Kama kazi unayofanya haiwasaidii watu basi inawaumiza, na kwa kufanya kazi ya aina hiyo, huwezi kupata mafanikio makubwa.
Kama biashara unayofanya haisaidii watu, basi inawaumiza, na kwa aina hiyo ya biashara usijioteshe kwamba siku moja utakuwa na mafanikio makubwa.
Kama unaona kuna watu wanaumia mahali, na wewe una uwezo wa kuwasaidia, kama utaona sio jukumu lako na hivyo kutokuwasaidia basi na wewe umechangia kuwaumiza.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, hakikisha upo kwenye upande wa kuwasaidia wengine na sio kuwaumiza.
Kwa sababu mafanikio yako yanategemea sana mafanikio ya wengine, ukishakuwa kwenye upande wa kuumiza watu, huwezi kupata mafanikio. Na hata ukiyapata yatakuwa ya muda mfupi tu, hayatadumu.
SOMA; BIASHARA LEO; Kama Huwezi Kusema Kitu Hiki Kimoja, Huna Biashara.
TAMKO LANGU;
Nimejua ya kwamba naweza kuwa nawasaidia watu au naweza kuwa nawaumiza, hakuna kati kati kwenye hilo. Mimi nimechagua kuwasaidia watu kwa sababu najua mafanikio yangu yanategemea mafanikio ya wengine. Nitafanya kila ninachoweza kufanya, kuhakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora sana, na yangu yatakuwa bora zaidi.
NENO LA LEO.
The purpose of human life is to serve, and to show compassion and will to help others – Albert Schweitzer
Dhumuhi kuu la maisha ya mwanadamu ni kuhudumia, na kuonesha huruma na kuwa tayari kuwasaidia wengine.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.