Au mwezi ujao, au mwaka ujao.
Ukweli ni kwamba tunapojua kwamba tunahitaji kufanya mabadiliko kwenye maisha yetu, na wakati huo tukawa hatupo tayari kufanya mabadiliko hayo, huwa tunatafuta sehemu ya kujificha.
Na sehemu rahisi sana ya kujificha ni kusema nitaanza vizuri wiki ijayo, au nitaanza vizuri mwezi ujao. Au mwaka unapoanza na mimi nitaanza.
Hii ni sababu ambayo wengi wanatumia kujificha, na kwa uzoefu wangu binafsi, wengi walioniahidi wangeanza kitu baada ya muda fulani hawakuwahi kuanza. Hata mimi mwenyewe nilipokuwa bado natumia kauli hiyo sikuwahi kufanya nilichokuwa nataka kufanya.
Kama kuna kitu muhimu kwako kufanya, anza kukifanya sasa, hata kama hujawa tayari, anza kufanya kwa hatua ndogo, au hata kupata taarifa muhimu. Ukiacha kuanza kwa kisingizio kwamba utaanza vizuri baada ya muda fulani, hutaanza kabisa, na utaikosa fursa nzuri ya kuboresha maisha yako.
Umefika wakati sasa uache kujidanganya na kuwa mkweli, kama hupo tayari kwa kitu jiambie tu sipo tayari na sifanyi, ili kama ni muhimu ujue kabisa kwamba unakikosa. Ila kujiambia utaanza baada ya muda fulani, ni kupunguza yale maumivu ya kutokufanya.
Kuna vitu vingi unavichelewesha makusudi ili usivifanye. Kwa hakika havihitaji muda ziadi, ni wewe kuanza kufanya pale unapopata wazo la kufanya. Vitu kama kubadili mlo wako, kufanya mazoezi, kujifunza zaidi, kuweka juhudi kwenye kazi au biashara yako, kuanza biashara, kuboresha mahusiano yako, kujenga nidhamu ya fedha na muda, KUSEMA HAPANA.
Kusema utaanza baada ya muda fulani, ni kutoroka au kukimbia kutokufanya kabisa. Anza kufanya sasa, kwa kile ulichonacho sasa.
SOMA; Mambo Matano(5) Muhimu ya kuzingatia kama umepanga kuanza biashara 2016.
TAMKO LANGU;
Najua ya kwamba nimekuwa najidanganya kwamba mabadiliko ninayotaka kufanya kwenye maisha yangu nitaanza baada ya muda fulani. Ila muda huo umekuwa unapita na nakuwa sijaanza kufanya mabadiliko hayo. Sasa nimeamua kuacha kujidanganya na kuanza kufanya jambo pale ninapopata wazo au ninaposhawishika nahitaji kubadilika. Sitaki tena kupoteza muda.
NENO LA LEO.
“You can dance in the storm. Don’t wait for the rain to be over before because it might take too long. You can can do it now. Wherever you are, right now, you can start, right now; this very moment.”
― Israelmore Ayivor
Unaweza kucheza kwenye dhoruba. Usisubiri mpaka mvua zikatike, kwa sababu zinaweza kuchukua muda mrefu. Unaweza kuanza sasa. Pale ulipo, sasa hivi, unaweza kuanza. Anza sasa.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.