Kuna wakati ambapo wafanyabiashara huwa tunajisahau sana. Tunapitiwa kwa kufikiri kwa kuwa sisi tunaijua biashara yetu basi mteja naye anajua. Au tunafikiri kwa sababu tumeshaeleza kwa wateja basi ni jukumu la kila mteja kujua.

Ni jukumu lako wewe kumweleza kila mteja kuhusu biashara yako, na sio wote watakaokuelewa. Hivyo kuwa tayari kujibu maswali ya mambo ambayo umeshayaeleza tayari.

Mara nyingi wafanyabiashara huulizwa maswali na wateja na kuona kama wateja wanataka tu kuwakomoa. Unaona swali gani hilo la kuuliza wakati nimeshakwambia. Wakati mwingine unamjibu vibaya.

Lakini ukweli ni kwamba wewe ndiye unayeijua biashara yako, na sio mteja wako. Hivyo hata kama umeeleza mara ngapi, kuwa tayari kueleza tena pale mteja anapouliza.

Toa maelezo mazuri ya biashara yako kila mara na wateja wataielewa vizuri na kuendelea kufanya biashara na wewe.

Kila la kheri.

MUHIMU; Kama una swali, maoni au changamoto yoyote ya kibiashara, weka kwenye maoni hapo chini na tutajadiliana zaidi na kama itahitajika nitaandaa makala ya kuhusu jambo hilo kwenye makala zijazo.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz