Tunapenda kubadili maisha yetu, ili yawe bora zaidi na tuweze kufikia mafanikio makubwa. lakini wengi wanashindwa kwenye hatua za kwanza kabisa, kwa sababu hawajui nguvu yao ilipo.
Jamii imekuwa inapotosha sana kuhusu nguvu zako zilipo. Utaambiwa mambo mengi sana, lakini siyo ya kweli. Mambo haya mengi tunayoambiwa ndiyo yanatufanya tuone hatuna nguvu ya kufanya makubwa. kwa sababu labda tumetokea familia masikini, au hatukupata elimu kubwa, au hatuna mtandao mkubwa wa watu wenye uwezo na mengine mengi.
Ni kweli mambo hayo yanaweza kuwa muhimu sana kwako kufikia mafanikio makubwa, ila hayawezi kuchukua nafasi muhimu sana ya nguvu yako. nguvu yako ndiyo hatua ya kwanza kabisa kwako kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa kama unavyotaka mwenyewe.
Wengi hawajui nguvu hii iko wapi, leo wewe unajua na utaanza kuitumia nguvu hii.
Nguvu yako ua kuyafanya maisha yako kuwa bora, ipo ndani yako mwenyewe. Nguvu hii unayo hapo ulipo, bila ya kujali upo chini kiasi gani au umetokea wapi. Nguvu hii imelala usingizi na inakusubiri wewe uiamshe na kuanza kuitumia. Na unaiamsha nguvu hii pale unapojua ni nini hasa unachotaka na kujitoa kwa kila hali kuhakikisha unapata hiko unachotaka. Hapa utaona nguvu ya ajabu ikikusukuma kufikia kile ambacho unakitaka.
Nguvu ipo ndani yako, iamshe na itumie kuwa na maisha bora sana akama ambavyo wewe mwenyewe unataka. Mambo mengine ya nje ni muhimu, ila lazima nguvu hii iwepo ili hayo ya nchi uweze kuyatumia.
SOMA; Maeneo matatu ya kuongeza nguvu kwenye biashara yako mwaka huu 2016.
TAMKO LANGU;
Najua ya kwamba nguvu kubwa ya kubadili maisha yangu ipo ndani yangu. Nitaitumia nguvu hii vyema ili niweze kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa. najua vitu vingine vya nje ni muhimu, ila vinahitaji nguvu iliyopo ndani yangu ndio viweze kunisaidia.
NENO LA LEO.
“The greatest discovery of all time is that a person can change his future by merely changing his attitude.” ~ Oprah Winfrey
Ugunduzi mkubwa kuwahi kutokea ni mtu anaweza kubadili maisha yake kwa kubadili mtazamo wake.
Nguvu kubwa ya kubadili ipo ndani yako, anza kuitumia ili uwe na maisha bora na ya mafanikio.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.