Kuna njia nyingi sana unazoweza kutumia kuua biashara yako.
Kwanza elewa kwamba wewe mwenyewe ndiye utakayeua biashara yako. Siyo mtu mwingine yeyote, ni wewe kwa kufanya au kutokufanya mambo fulani kwenye biashara yako.
Sasa turudi kwenye hiki tulichopanga kujadili leo.
Njia rahisi sana ya kuua biashara yako ni kuacha kujali kuhusu wateja wako.
Pale unapoanza kuwazoea na kuona kuja kwao kwenye biashara yako ni kwa shida zao, hapo unakuwa umeweka sahihi kwenye kifo cha biashara yako.
Na mazoea huwa yanaanza taratibu,
Pale unapokosa muda wa kuwajibu wateja wako vizuri,
Pale unapokataa kumsaidia mteja wako anapopata changamoto kupitia biashara yako.
Pale unapomwambia mteja kama hutaki unaweza kununua kwa mwingine.
Pale mteja anapoongea na wewe na unaendelea kuwa ‘bize’ na simu yako.
Najua unaendelea kupata mengi yanayoendana na hilo, yajazie hapo.
Na kama unataka biashara yako ife fanya mambo hayo. Kama unataka istawi basi kila siku pigana kukwepa mambo hayo.
Mfanye mteja ajisikie vizuri anapokuwa kwenye biashara yako. Kwa kuhakikisha unampatia huduma bora sana.
Nakutakia kila la kheri,
Kocha.