Biashara inaonekana rahisi pale unapofikiria kununua na kuuza pekee.

Au kuandaa bidhaa au huduma yako kisha kusubiri wateja waje wa nunue.
Lakini biashara siyo rahisi hivi, na ndio maana wengi wanashindwa.
Kwa sababu huwa wanafikiri ukishakuwa na mtaji tu unaendesha biashara.
Kinachoongeza ugumu kwenye biashara ni ile hali kwamba wateja wako ni binadamu, na binadamu ni viumbe tata.
Kwanza kabisa mara nyingi kinachowasukuma watu kununua ni hisia.
Na hivyo kabla mteja hajanunua kile unachouza, anakununua wewe kwanza.
Ni lazima akukubali wewe ndiyo aweze kufanya biashara na wewe.
Ni lazima aone unamjali, aone upo kwa ajili yake na ajisikie anakaribishwa kwenye biashara yake.
Hujawahi kuona sehemu kuna biashara zinafanana, lakini kwa mmoja watu wamejaa na kwa mwingine hakuna mtu kabisa?
Sasa kama huijui vizuri sayansi ya biashara utasema anatumia dawa, au nguvu za tofauti.
Lakini ukweli ni kwamba mtu yule ameweza kujiuza yeye mwenyewe kwanza na hivyo watu kumkubali.
Jione wewe kama bidhaa na jiweke kwenye hali ambayo wateja wako watakununua.
Na kumbuka mara zote kuwa kwenye hali hiyo ili uendelee kuijenga na kuikuza biashara yako.
TUPO PAMOJA.
Kocha.
Kwa lolote kuhusu biashara tafadhali andika kwenye maoni hapo chini.