Dunia imekuwa inatudanganya kitu kimoja, ya kwamba fursa zipo nje yetu na hivyo ni sisi kuhakikisha tunazitafuta na kuzitumia.
Ukweli ni kwamba fursa hazipo nje yetu bali zipo ndani yetu.
Tunapozijua fursa zilizopo ndani yetu,mkitu chochote kinachotuzunguka kinakuwa fursa kubwa kwetu.
Tutaweza kukitumia na kuweza kufanya mambo makubwa.
Lakini kama hatutaijua fursa iliyopo ndani yetu na jinsi ya kuweza kuitumiam tutajikuta tunahangaika na kila tunayoambiwa ni fursa lakini hatupati kile ambacho tunakitaka.
Fursa nyingi za kufanikiwa kibiashara zinaanza na wewe hapo ulipo, na hatimaye unaweza kuitumia biashara yako vizuri ili kufikia mafanikio makubwa.
Kabla hujaanza kutafuta ni biashara ipi nzuri kuliko hiyo unayofanya sasa, hebu fungua akili yako na iangalie biashara unayoifanya sasa kwa undani zaidi. Angalia ni maeneo gani ambayo unaacha fedha iondoke.
Ukitaka kuona vizuri iangalie biashara yako kama mtu ambaye anataka kuja kuanza biashara kama yako na hapo ulipo. Anza kuwa mshindani wako mwenyewe na utaziona fursa nyingi zaidi. Siyo kwamba fursa hizo hazikuwepo, bali wewe hukuwa umejua fursa inaanzia ndani yako.
Fursa zinaanza na wewe, chukua hatua na utakuza biashara yako.
Kila la kheri.