Kilichotufanya sisi binadamu kufika hapa tulipo, ni ubora wetu.

Mwanasayansi Charles Darwin, katika kanuni yake mageuzi katika viumbe hai, alisema kwamba wale viumbe ambao wameweza kuyamudu mazingira yao vizuri, ndiyo walioweza kupona na kuzaliana. Kwa Kiingereza hii inaitwa ‘survival of the fittest’

Katika kanuni yake hii Darwin alisema kwamba viumbe wengi sana wanazaliwa lakini siyo wote wanaoweza kukua na kufikia hatua ya kuzaliana. Wengi wanaishia katikati kwa sababu wanakuwa hawajayamudu mazingira yao vizuri. Wale wanaoyamudu wanakua na kuzaliana na hivyo kuendeleza ule ubora wao.

Kanuni hii inaeleza mambo yanayotokea kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kwa mfano, watu wengi sana wanaingia kwenye biashara kila siku, lakini siyo wote wanaoweza kukuza biashara zao, wengine wengi wanaishia njiani.

Watu wengi wanaanza kazi pamoja, lakini baada ya muda utakuta wachache wameweza kuwa na maisha mazuri na wengine wengi wana maisha ya hovyo.

Kitu kikubwa kinachotofautisha watu ni ubora, yule ambaye yupo bora kwenye kile anachofanya, ndiye anayepona na kufanikiwa. Yule ambaye anaweza kuyatumia vizuri mazingira yanayomzunguka, ndiye anayepata fursa nzuri zinazomletea mafanikio.

SOMA; Kwa Mabadiliko Yanayoendelea Nchini, Ni Lazima Tubadili Mbinu Zetu Za Kibiashara Kama Tunataka Kufanikiwa.

Sasa kazi ni kwako kuchagua, unataka kuwa bora na ufikie mafanikio au unataka kuwa kawaida na upotezwe kabisa. Kama unataka kufanikiwa ni lazima uwe bora sana kwenye kile ambacho unakifanya. Lazima uwe na njia ya kukutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanajaribu kufanya kile ambacho wewe unafanya.

Hakuna kitu rahisi, ili upone ni lazima uweo tofauti, lazima uwe bora na lazima uweze kuyamudu mazingira yako. kuwa bora leo na kila siku.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)