Moja ya vitu ambavyo unahitaji kwenye biashara ni kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi. Na taarifa hizi zitakuwezesha wewe kufanya maamuzi sahihi kwa pale ulipo kibiashara ili kuweza kusonga mbele zaidi.
Mafanikio ya biashara yanategemea wakati uliopo na kile unachofanya. Kwa mfano mtu aliyekuwa anajua matumizi ya kompyuta wakati zinaingia kwa wingi, aliweza kutengeneza biashara nzuri wakati huo.
Pale ambapo kuna ugunduzi mpya, watu wanaweza kutengeneza biashara mpya. Pale ambapo mabadiliko yanaendelea, fursa nyingi za kibiashara zinaibuka.
Kwa kuwa mabadiliko yanaendelea kutokea kila siku, hakikisha wewe una taarifa sahihi ili uweze kuzitumia kufanya makubwa. hapo ulipo sasa ni sahihi, sasa unahitaji kujua kipi sahihi kufanya kwa hapo ulipo sasa. Utajua kama ukiwa mdadisi na mfuatiliaji wa kile unachofanya.
Huhitaji kwenda mbali ndiyo uzione fursa, bali hapo ulipo umezungukwa na fursa nyingi kama ukiweza kuziona na kuanza kuzitumia.
Nakutakia kila la kheri katika ukuaji wa biashara yako.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
MUHIMU; Kama una swali, maoni au changamoto yoyote ya kibiashara, weka kwenye maoni hapo chini na tutajadiliana zaidi na kama itahitajika nitaandaa makala ya kuhusu jambo hilo kwenye makala zijazo.
Kwa ushauri wa moja kwa moja kuhusu biashara yako kutoka kwangu bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.