Vitu tunavyotaka kukamilisha kwenye maisha yetu, vipo ndani ya uwezo wetu.
Vile ambavyo tunataka kuwa kwenye maisha yetu ipo ndani ya uwezo wetu.
Malengo makubwa ambayo tunataka kuyafikia kwenye maisha yetu, yapo ndani ya uwezo wetu.
Ndoto kubwa tunazoota kwenye maisha yetu, taswira ya amisha bora tunayoipata ni kitu ambacho tunaweza kufikia.
Lakini tatizo ni moja, kufikia haya makubwa tunayotaka, tunahitaji kupita kwenye njia itakayotupeleka huko.
Tatizo kubwa zaidi ni kwamba njia hii ni ngumu, imejaa mateso, inakera, inakatisha tamaa na inasababisha kuvurugikiwa. Ni njia ambayo siyo rahisi hata kidogo, na ili mtu uweze kufikia kule unakotaka, ni lazima uwe umejitoa kweli.
Kitu chochote ambacho ni kizuri na tunakithamini, kuna gharama lazima tulipe ili tuweze kuwa nacho. Hivyo kupata yale makubwa unayotaka, jiandae kuteseka zaidi ya ulivyozoea.
Swali linalobaki kwako siyo kama inawezekana wewe kufikia mafanikio makubwa au la. Bali swali ni je upo tayari kuteseka? Na upo tayari kuteseka na nini? Kama haupo tayari kuteseka, sahau kuhusu mafanikio.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)