Tunahitaji sana ubunifu kwenye maisha yetu ya kila siku. Kwa chochote tunachofanya kwenye maisha yetu, tunahitaji ubunifu ili kupata matokeo bora na ya tofauti. Ni kupitia matokeo haya ndiyo tunaweza kujijengea mafanikio makubwa.

Pamoja na juhudi kubwa tunazoweka ili kuwa na ubunifu, kuna vitu ambavyo vimekuwa vinaua ubunifu wetu. Vitu hivi vinaanza na sisi wenyewe kabla hata hatujamnyooshea kidole mtu mwingine. Ni muhimu kujua vitu hivi ili visiendelee kuturudisha nyuma.

Vifuatavyo ni vitu ambavyo vinaua ubunifu wetu;

  1. Woga na hofu. Unapokuwa na hofu huwezi kuwa mbunifu, hofu inazuia akili yako kuja na mawazo ya kibunifu.
  2. Msongo wa mawazo. Kama una msongo wa mawazo, ni vigumu sana kuweza kuituliza akili yako na kuja na mawazo ya kibunifu. Mara zote utakuwa unafikiria yale yanayokuletea msongo.
  3. Njaa, ukiwa na njaa unachofikiria ni chakula zaidi.
  4. Uchovu. Unapokuwa umechoka, akili yako haitaki kujisumbua kufikiria, hivyo huwezi kuja na mawazo ya kibunifu.
  5. Kiu, sawasawa na njaa.
  6. Shinikizo. Mtu anayefanya kitu kwa shinikizo ni vigumu kuja na mawazo ya kibunifu.
  7. Kuwa na mambo mengi kwa wakati mmoja. Kujaribu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja akili yako inakuwa imejaa na hivyo kushindwa kuja na mawazo ya kibunifu.

SOMA; BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kukabiliana Na Anayekuiga Kwenye Biashara.

Ili kuiruhusu akili yako iweze kuja na mawazo ya kibunifu, hakikisha mwili wako na mazingira yako yapo tulivu. Akili inapokuwa tulivu inakuwa na nafasi ya kuja na mawazo ya kibunifu.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)