Kuna suluhisho la kila tatizo ambalo watu wanapitia.

Na pia kuna tatizo kwenye kila suluhisho ambalo watu wanapata kuhusu matatizo yao.

Vyote viko pale, ila wewe ndiye unayechagua kipi unataka kuona.

Watu wanaoshinda na kufanikiwa, mara zote wamekuwa wanaona suluhisho kwenye kila tatizo. Wakishaliangalia tatizo akili zao zinakwenda moja kwa moja kwenye suluhisho.

Watu wanaoshindwa na kutokufanikiwa, mara zote wamekuwa wanaona tatizo kwenye kila suluhisho. Wakishaangalia suluhisho akili zao zinakwenda moja kwa moja kwenye tatizo la suluhisho hilo.

Uzuri wa akili zetu ni kwamba zinatuwezesha kuona kile ambacho tunataka kuona. Na mawazo yetu yako vizuri sana kutuletea kile ambacho tunakifikiria kwa muda mrefu. Hivyo kama umekuwa unafikiria suluhisho, kila mata utakuwa unaona suluhisho. Kama umekuwa unafikiria matatizo, kila mara utakuwa unaona matatizo.

SOMA; KURASA ZA MAISHA; Mtazamo Mpya Wa Maisha Ya Furaha Na Mafanikio.

Je ni kipi ambacho unaona zaidi kwa sasa? Matatizo au suluhisho?

Uzuri ni kwamba tunaweza kubadili maisha yetu kwa kubadili mtazamo ambao tunao kuhusu maisha yetu. Hivyo kama umekuwa mtu wa kuona matatizo pekee, unaweza kubadili mtazamo wako na kuanza kutafuta suluhisho kwenye kila jambo.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)