Fanya unachotaka kufanya, hakuna wa kukuzuia.
Kile unachofikiria kufanya, kikwazo ni wewe mwenyewe.
Hofu unaweza kujijaza, watu watanichukuliaje?
Unachosahau ni kwamba, kila mtu anawaza yake.
Badala ya kupoteza muda kuwaza, panga na anza kufanya.
Hata kama huna uhakika, anza na utaona njia zaidi.
Muhimu siyo kusema unafanya, bali kufanya kwa hakika.
Leo nimeamua kuandika shairi, sijawahi kuandika awali,
Sifati sheria yoyote, sio kina wala kirai.
Nafanya ninachotaka kufanya, kwa kuwa hakuna wa kunizuia.
FANYA UNACHOTAKA KUFANYA…
#KochaMakirita
http://www.makirita.info