Habari za leo rafiki?
Ni mimi rafiki na kocha wako, Makirita Amani,
Kila siku nimekuwa nakuandikia makala kuhusu maisha, biashara na mafanikio kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Nina habari kubwa sana kwako, ambazo unahitaji kusikiliza kwa makini ili uweze kuchukua hatua.
Mpaka kufikia sasa, zimebaki siku 120 ili kumaliza mwaka huu 2016.
Mwaka huu 2016 ulipoanza, uliweka malengo makubwa ya kutimiza mwaka huu. Ni kawaida kwa kila mtu kuweka malengo iwe kwa kujisemea au kwa kuyaandika kabisa.
Takwimu zimekuwa zinaonesha kwamba asilimia 80 ya watu wanaoweka malengo yao wanakuwa wameshayasahau baada ya miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka.
Wale wanaobaki ni wachache sana wanaoweza kuyafikia malengo yao, wengi wamekuwa wakishindwa kuyatimiza, na wengine wengi wamekuwa hata hawayaanzi kabisa.
Najua kwa sababu fulani fulani, kuna malengo yako uliyojiwekea mwaka huu 2016 ambayo bado hujaweza kuyatekeleza. Huenda umeanza lakini hujafika mbali, au hata hujaanza kabisa.
Ili kuhakikisha kwamba mwaka huu hauishi hivi hivi, nimekuandalia program nzuri inayokwenda kwa jina la SUPERCOACHING.
SUPERCOACHING ni nini?
Supercoaching ni nafasi ya wewe kufanya kazi na mimi bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo yako ya mwaka huu 2016 ndani ya siku 120 zilizobaki kwenye mwaka huu, hata kama hujaanza kabisa.
Ni nini tunafanya kwenye supercoaching?
Kwanza kabisa unayaandika malengo yako yote uliyojiwekea kwa mwaka huu 2016, kisha unachagua lengo moja kubwa na muhimu sana. Lengo hili liwe ambalo ukilitimiza au ukianza kulifanyia kazi basi unabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Pili tunaanza kulifanyia kazi lengo hilo moja pekee, kwa kuweka kila sababu pembeni, unajitoa kufanya chochote kinachowezekana ili mwaka huu 2016 unapoisha, basi uweze kusema kuna hiki nilifanya.
Hatari ni kwamba, kama utaendelea kwenda kama unavyoenda sasa, kuna malengo ambayo hutayafikia, na hivyo siku hizi 120 zilizobaki utashangaa zinaisha ukiendelea kuwa hapo ulipo sasa.
Hivyo unahitaji kufanya kitu cha ziada, unahitaji kufanya kitu cha tofauti na ulivyokuwa unafanya kwenye siku 245 zilizopita kwenye mwaka huu. Peke yako huwezi kufanya hivyo ndiyo maana nimesogea karibu yako, ili tuweze kwenda pamoja.
Supercoaching inaendeshwaje?
Mimi na wewe tutajadili lile lengo ambalo unataka kulifanyia kazi kwa mwaka huu, inawezekana ulipanga kununua shamba/kiwanja, inawezekana ulipanga kuanza ujenzi, inawezekana ulipanga kununua gari, au ulipanga kuanza kuandika vitabu. Huenda ulipanga kuanzisha blog, au kuanza biashara, au kukuza biashara yako zaidi. Huenda ulipanga kuanza ujenzi, au kupeleka kazi zako kwenye viwango vya juu zaidi.
Napenda kukuambia kwamba chochote ulichopanga kufanya mwaka huu, kinawezekana na utaanza kukifanya kama utajiunga na program hii ya supercoaching.
Baada ya kujadili kwa pamoja na kupanga utekelezaji, mimi nitakuwa nakufuatilia, kila wiki tutakuwa na mazungumzo kwa njia ya simu, ambapo unanipa mrejesho umefikia wapi kwa kadiri tulivyoweka mipango. Pia mara kwa mara nitakuwa nakutafuta kujua unafanya nini kwa wakati husika. Kwa kifupi nitakufuatilia sana kuhakikisha hurudi tena nyuma.
Mahitaji ya kujiunga na Supercoaching;
- Uwe na malengo, na uwe na lengo moja kubwa ambalo unataka kulitimiza kwa mwaka huu.
- Uwe umeshachoka na hapo ulipo, uwe tayari kufanya chochote unachoweza kufanya ili kutoka hapo ulipo.
- Usiwe mtu wa kutafuta sababu, uwe mtu wa kutafuta suluhisho pale unapokwama. Ukiendekeza sababu programu hii itakushinda.
- Uwe unaamini kwamba kile unachotaka kinawezekana, na upo tayari kuweka juhudi, pia uwe unafundishika na kufanyia kazi makubaliano ambayo tunawekeana.
- Uwe tayari kugharamia huduma hii, japo gharama ni ndogo sana, lengo la gharama hii ndogo ni kuwapunguza wale ambao hawapo serious, ambao hawapo tayari kweli kuchukua hatua za kubadili maisha yao.
Karibu kwenye Supercoaching,
Hii ni programu ambayo nina uhakika kwa asilimia 100 itakwenda kuacha alama kwenye maisha yako. Na kama kwa namna yoyote ile hutapata matokeo mazuri, nitakurudishia gharama yote utakayokuwa umeingia kwa kulipia program hii. Chukua maneno yangu, ni sheria, nitakurejeshea gharama zako kama hutaridhika.
Nafasi ni chache sana, hivyo kama umesoma hapa na kuelewa, chukua hatua mara moja, maana ukichelewa utaikosa nafasi hii.
Kupata nafasi ya kushiriki SUPERCOACHING jaza fomu hiyo hapo chini.