Kila mmoja wetu kuna wakati ambao anapitia mambo magumu kwenye maisha yake. Wakati ambao unakutana na changamoto na kuona hakuna tena njia nyingine ya kwenda. Nyakati kama hizi ni ngumu sana na haijalishi wewe ni nani, zinaumiza.
Tunapokuwa kwenye nyakati kama hizi, ni rahisi sana kukata tamaa, kwa sababu kwa kawaida yetu binadamu, tumekuwa tunaangalia zaidi yale mabaya kuliko mazuri. Kwa kuwa nyakati kama hizo tunakuwa tunapitia mabaya, basi tunaona mabaya zaidi yakija.
Njia bora ya kuvuka kwenye nyakati hizi ngumu, ni kuangalia ni kipi unaweza kufanya kwa wakati huo. Sawa mambo ni magumu, ndiyo unapitia changamoto nyingi, lakini ni hatua zipi unazoweza kuzichukua kwa wakati huo na ukaanza tena kupiga hatua?
Hapa ndipo pa kuanzia. Na kwa uhakika ni kwamba, yapo mambo mengi unayoweza kuanza kufanya na kuondoka kwenye hali ngumu unayopitia. Angalia ni yapi unaweza kudhibiti, angalia ni yapi ukifanya utaleta matokeo ya tofauti, kisha fanya hayo. Usiruhusu akili yako irudi kwenye kufikiria yale mabaya pekee, idhibiti kuona yale ambayo unaweza kufanya kwa wakati huo na yafanye.
Ni kwa njia hii unaweza kuondoka kwenye magumu na changamoto yoyote, na kuweza kuyajenga maisha yako upya. Hivi ndivyo watu wanavyotoka sifuri mpaka mafanikio.
Je ni hatua zipi unazoweza kuchukua sasa ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi?
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK