Kila tunachofanya kwenye maisha yetu, kina mchango kwenye mafanikio yetu. Inawezekana kuwa mchango chanya au mchango hasi. Inategemea ni nini umefanya na umefanya kwa kusudi gani.
Pamoja na kila kitu kuwa na mchango wake, bado michango ya vitu unavyofanya haifanani. Kuna vitu ukifanya vina mchango mkubwa wakati vingine vina mchango kidogo sana.
Leo tunakwenda kuangalia tofauti ya hivi tunavyofanya kwa michango yake.
Asilimia 1.
Kuna vitu vingi ambayo tumekuwa tunafanya, ambavyo vina mchango mdogo sana, wa asilimia moja kwenye mafanikio yetu. Changamoto kubwa ni kwamba sisi wenyewe tumekuwa hatujui mchango wake ni kidogo.
Kwa mfano, kupanga, kupanga ni muhimu sana, lakini hata uwe na mipango mizuri kiasi gani, haitaweza kukutoa hapo ulipo sasa. Vitu vingine ni kama kukubali mambo madogo madogo yakuzuie kuanza. Mfano kulalamikia ukosefu wa mtaji, au kujiona bado hupo tayari. Inaweza kuwa kweli, lakini mchango wake kwenye mafanikio yako ni kidogo sana.
Asilimia 99.
Kuna vitu ambavyo ukifanya vinaleta matokeo makubwa sana, au vinakuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata matokeo bora baadaye. Vitu hivi ni kama kuchukua hatua na kufanya, kuanza hata kama bado hujawa tayari, kutumia mazingira yanayokuzunguka kupata nafasi ya kuanzia.
Chochote kile kinachohusisha kufanya, kipo kwenye kundi la asilimia 99. Chochote kile kinachokufanya uchukue hatua, na siyo tu kusema na kupanga, kipo kwenye kundi la asilimia 99.
Hatua ya kuchukua.
Fanya zaidi yale yaliyo kwenye kundi la asilimia 99, lakini pia usisahau yaliyopo kwenye kundi la asilimia 1.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK