Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa asubuhi nyingine nzuri ya leo ambapo tunapata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tumechagua kufanya. Tutumie nafasi hii vizuri rafiki.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu TIME MANAGEMENT,
Wote tunajua namna muda ulivyo adimu, namna mafanikio yetu yanavyotegemea muda.
Lakini kila mmoja wetu bado anateseka na kudhibiti na kusimamia muda wake.
Hii ni kwa sababu tunapojatibu kudhibiti na kusimamia muda, hatujui ni wapi sahihi pa kufanya hivyo.
Kwa mfano huwezi kudhibiti muda, hii ni kwa sababu muda hauwezi kuongezeka, tuna masaa 24 pekee kwenye siku, hata ufanye nini, huwezi kuongeza hata sekunde moja.

Tunachoweza kudhibiti na kusimamia vizuri ni matumizi yetu ya muda. Hapa ndipo tunaweza kuhakikisha tumetumia muda wetu vizuri kwa ajili ya mafanikio.
Katika matumizi yetu ya muda kuna kitu kinaitwa PRIORITY, lazima tuwe na vipaumbele kwenye matumizi yetu ya muda. Bila ya vipaumbele utajikuta umeimaliza siku yako, umechoka kabisa, lakini huoni jambo kubwa ulilofanya.
Bila ya kutangeneza na kusimamia vipaumbele vyako, utajikuta muda wote muda wako umejaa na huoni hatua kubwa unazopiga.
Hivyo rafiki yangu, badala ya kupambana na kumanage time, hebu anza kumanage priority zako mwenyewe.

Ianze siku yako kwa kufahya yale ambayo ni kuhimu ziadi kabla ya kufanya mengine ya kawaida. Usikubali kuyumbishwa yumbishwa kama bendera, fanya yale ambayo ni muhimu kwako.

Nakutakia siku njema sana rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
Contacts; +255 717 396 253 / makirita@kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.

img_20161112_091656