Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta kwa muwa mrefu lazima utakuwa unajua kwamba programu za kompyuta kuna wakati huwa zinakuwa zimepitwa na wakati. Kwa neno la kingereza wanasema OUTDATED. Angalia mfano programu kuu ya kuendesha kompyuta inayoitwa windows, zimekuwepo nyingi na zote zinapitwa na wakati na hivyo kuja nyingine.

Mfano kulikuwa na windows 95, ikaja windows 98, ikaya windows 2000, ikaja windows xp, ikaja windows vista, ikaja windows 7, baadaye windows 8 na sasa windows 10. Kwa kipindi cha kama miaka 20 program ya windows imeshabadilishwa na kuboreshwa zaidi ya mara 8.
Kama pia unatumia simu na unatumia programu (apps) mbalimbali, utakuwa unaona kwamba kila mara wanakuambia UPDATE. Kwa mfano kama unatumia wasap, kuna kipindi unaambiwa wasap yako ipo outdated na hivyo unatakiwa ku update.
Sasa leo kwa dhana hii hii nataka nikuoneshe ni kwa namna gani akili yako imepitwa na wakati, yaani ipo OUTDATED na unapaswa kuiUPDATE leo na kila siku ya maisha yako.
Kama unafanya kazi zako kila siku kwa mazoea, miaka kwa miaka sasa, akili yako imepitwa na wakati.
Kama unafanya biashara zako leo kama ulivyokuwa unafanya jana na siku zilizopita, ni wakati sasa wa ku update akili yako.
Kama unaendesha maisha yako kwa mazoea, kama ambavyo kila mtu anayaendesha kwenye jamii, upo nyuma sana kiakili na kimafanikio pia.
Kama ilivyo kwa program za kompyuta na simu, akili zetu ndiyo kompyuta kubwa kabisa kwenye maisha yetu. Ndiyo kompyuta inayoweza kutuletea chochote tunachotaka. Lakini kama kompyuta hii haitapata huduma ya mara kwa mara, itapitwa na wakati na itashindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Je unawezaje ku update akili yako?
Njia ya kwanza kabisa ni kujifunza kitu kipya kila siku, na kujiwekea utaratibu wa kuchukua hatua yoyote kutokana na kile ulichojifunza. Hata kama ni hatua ndogo sana, kikubwa ni uchukue hatua kutokana na taarifa mpya ulizopata. Kila siku soma vitabu, kila siku tafakari maisha unayopitia na kila siku waangalie wengine na jifunze kupitia wao.
Njia ya pili ni kuwa mbunifu. Usikubali kufanya kitu kwa njia zile zile ulizozoea kufanya kila siku. kila siku kuwa mbunifu, tafuta mbinu mpya na bora zaidi za kufanya. Usifanye tu kwa sababu unafanya, bali kila siku jiulize ni njia gani bora zaidi ya kufanya na jaribu njia hizo.
Tatu, kuwa tayari kukosea. Katika kujifunza na kujaribu vitu vipya, kuna mahali utakosea. Ili uweze kuwa up to date yaani kwenda na wakati, lazima uvuke hofu ya kukosea ili uwe huru kufanya mambo mageni na makubwa.
Ifanye akili yako kwenda na wakati kila siku, KILA SIKU, kwa kujifunza mambo mapya, kuwa mbunifu na kuwa tayari kukosea.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK