Hongera rafiki yangu kwa asubuhi nzuri ya leo.
Tumepata tena nafasi bora ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile tukichochagua kufanya.
Rafiki yangu, kaitumia nafasi ya leo vizuri ili uweze kufanya makubwa.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu DENIAL, au KUKATAA UHALISIA…
Kuna wakati ambapo tunaouona uhalisia kama ulivyo, ila kwa kuwa hatutaki kuuona kama ulivyo, au hayutaki kuchukua hatua, basi tunajifanya kama hatujauona.
Tunajua kabisa kwamba tunaendesha biashara zetu kizembe, tunajua kuna mambo tulipaswa kuyafanya lakini hatutaki kuyafanya, na hivyo tunajikania wenyewe kwamba hakuna uzembe wowote tunaofanya. Ni mpaka pale inapotokea changamoto kubwa ndipo tunaona athari za kutokuchukua hatua haraka.
Tunajua kabisa kazi tunazofanya hazitupi furaha na maana kwenye maisha yetu. Tunajua kabisa siyo kazi ambazo tunafurahia kufanya kila siku. Lakini hatuchukui hatua zozote kwa kujifanya kama hatuoni hilo, au kujifanya siyo tatizo kubwa.
Katika maisha yetu ya kila siku, yapo mambo mengi mno ambayo tunayaona na tunajua hayajakaa sawa, lakini tunajifanya kama vile hatujayaona, au tunafikiria hayataleta matatizo makubwa. Ni mpaka pale matatizo yanapotokea ndipo tunakumbuka tulikuwa na nafasi ya kuchukua hatua lakini hatukufanya hivyo.
Ufanye nini?
Kitu pekee cha kufanyw ni KUCHA KUJIFANYA KAMA HUJAONA.
Yaani ona kitu na epuka kujifanya hujaona. Ona kitu kama kilivyo kwa uhalisia wake, na acha kuijidanganya kwamba hakutakuwa na tatizo kubwa, au mambo yataenda vizuri yenyewe.
Kila kinachokuhusu wewe, wewe mwenyewe unahitaji kuchukua hatua ili mambo yaweze kwenda sawa.
Kama kuna kitu hakipo sawa, kifanyie kazi sasa, kabla hakijaleta madhara makubwa zaidi baadaye.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info