Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tulichopanga kufanya ili tuweze kupata matokeo makubwa zaidi.
Tutumie muda wetu wa leo vizuri rafiki kwa sababu ukishapita hauwezinkurudi tena.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KWENDA NA HALI ILIVYO (GO WITH THE FLOW).
Kama umejikuta katikati ya mawimbi makala ya maji, unaweza kuamua kuyaacha mawimbi yakupeleke popote yanapoenda, au unaweza kuamua kuweka juhudi za kupiga mbizi kuenda tofauti na mawimbi ili uende unakotaka wewe.
Ukiamua kufuata mawimbi hutumii nguvu yoyote, unapelekwa tu, ila tatizo hujui unapelekwa wapi.
Ukiamua kwenda kinyume na mawimbi utahitaji kutumia nguvu kubwa huku ukipata upinzani wa mawimbi, lakini utafika unakotaka kufika.

Hivyo ndivyo ilivyo kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.
Unaweza kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, ni rahisi lakini hujui mwisho ni wapi.
Au unaweza kufanya kile unachotaka wewe kufanya, ni ngumu lakini mwisho mzuri.
Chagua sasa, unafata mkumbo au unafanya yako?

Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info