Habari rafiki yangu,
Kama ambavyo nilikueleza kwenye makala iliyopita, leo tarehe 23/12/2016 ninaanza likizo yangu ya wiki moja, hivyo sitakuwa napatikana mpaka tarehe 30/12/2016. Hii ni wiki yangu moja ya kufanya makubwa bila ya usumbufu wa aina yoyote kutoka duniani.
Kama hukusoma makala ile na kujua kwa nini huwa najipa likizo hizi na nafanya nini, bonyeza maandishi haya kuna maelezo yote.
Kabla sijakushirikisha ujumbe wa leo, naomba nifanye masahihisho, kwenye makala iliyopita nilisema mwisho wa kulipia ada ya kushiriki ni tarehe 02/10/2017, hapo nilikosea, tarehe sahihi ni 02/01/2017. Hivyo fanya malipo yako mapema ili uweze kushiriki semina ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO. Kama ndiyo unasikia kuhusu semina hii kwa mara ya kwanza, basi bonyeza maandishi haya kupata taarifa zaidi.
Baada ya hayo mafupi nikukaribishe kwenye makala yetu ya leo fupi kabisa.
Katika makala hii nataka kukuambia ukweli ambao unaweza kukuumiza, lakini sina namna, inabidi tu ujue. Najua vizuri kitu cha mwisho ambacho mtu anapenda kusikia ni ukweli unaomuumiza. Lakini itabidi tu nikwambie ukweli ili kama utabaki hapa basi uwe mkweli.
Ujumbe ninaotaka kukuambia ni huu; MWAKA 2017 ITABIDI TU UKIMBIE MWENYEWE.
Kama ambavyo niliandika kwenye makala ya mambo matatu muhimu ya kufanya kwa mwaka 2017, nilishauri kama hujui ufanye nini, na kama bado hujaweza kuyasimamia maisha yako, na kwa namna yoyote ile utashindwa kushiriki semina yetu bora ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO, nilishirikisha vitu vitatu tu vya kufanya. Yaani nilisema 2017 tupa mbali kabisa malengo ambayo umekuwa unajiwekea halafu unayasahau, na ufanye vitu vile vitatu tu. Kama hukusoma makala ile na kujua vitu hivyo vitabu, bonyeza maandishi haya, utapata maelezo yote.
Sasa mmoja wa rafiki na msomaji mwenzetu, aliamua kunitolea uvivu na kuniandikia kuhusu makala ile. Na alinieleza wazi kabisa kwamba neno langu siyo sheria na sina mamlaka ya kuwapangia watu wafanye nini na maisha yao. Kila mtu anapaswa kufanya anavyotaka mwenyewe kwa sababu maisha ni yake mwenyewe.
Na ni kweli kabisa, msomaji mwenzetu yupo sahihi, neno langu halijawahi kuwa sheria hata siku moja kwa mtu mwingine zaidi yangu mwenyewe. Na ni kweli kabisa ya kwamba kila mtu anapaswa kufanya kile anachojisikia kufanya.
Lakini alichosahau rafiki yetu ni kwamba, kama njia unayotumia haikufikishi, na kama unachofanya hakileti matunda, na hakuna mfano wa ambaye amewahi kufanya akapata matunda, basi unapoteza muda wako. Ni bora kuangalia wengine wanafanya nini na wakasonga mbele na wewe ukafanya.
Kwa mfano, kukaa chini na kulalamika maisha magumu, mtaji hakuna na kadhalika, hakujawahi kumsaidia yeyote kufanikiwa. Sasa kwa nini unafikiri kutakusaidia wewe.
Hapa ndipo ninapotaka kuwakumbusha marafiki zangu wote kwamba mwaka 2017 sitakwenda kucheka na wewe. Binafsi huwa sipendi sababu sababu, hivyo kama mwaka 2017 utakuwa mtu wa sababu, kila ninachoandika kitaenda kukuumiza. Hivyo kama hupendi kusikia ukweli mchungu, nakushauri tu ukimbie mapema, maana mimi sitaacha kukuambia ukweli, sitakuja kukubembeleza kwa maneno ya uongo ya wanasiasa kwamba maisha yako ni magumu kwa sababu ya chama fulani, au kwa sababu hujapewa kitu fulani.
Mimi nakuambia na nitaendelea kukuambia hata kama utanishikia bastola ya kwamba kama maisha yako ni magumu, basi wewe mwenyewe umechangia ugumu huo. Na ni wewe mwenyewe unayepaswa kuchukua hatua ya kufanya maisha yako yawe bora. Siyo ndugu, siyo marafiki, siyo serikali wala mtu mwingine yeyote, ni wewe. Ukisoma mahali pameandikwa kinyume na hapo jua siyo maandiko yangu hayo. Msimamo wangu umekuwa huo siku zote na umeniwezesha kuchukua hatua kwenye maisha yangu, hata pale ninapokutana na changamoto kubwa.
Narudia tena rafiki, kama hutaki kusikia ukweli mchungu, kama hutaki mtu wa kukushushua na sababu zako za uongo ambazo umekuwa unajidanganya nazo miaka yote, basi kimbia haraka. Kuendelea kukaa na karibu na mimi mwaka 2017 utakuwa mchungu kwako.
Lakini pia utakuwa mtamu kwako kama utakuwa mtu wa kuchukua hatua, na utakuwa kwenye familia ya wana mafanikio ambao wameamua kushika hatamu za maisha yao.
Jinsi ya kukimbia.
Rafiki, kama unataka kukimbia kabla sababu zako za kupoteza mwaka 2017 sijaziharibu, basi acha kabisa kutembelea AMKA MTANZANIA na kama umepokea ujumbe huu kwa email basi shuka hapo chini kwenye email kuna sehemu imeandikwa UNSUBSCRIBE, ukibonyeza hapo tu umeshanifukuza kabisa, sitakusumbua tena na ukweli. Utaweza kujidanganya utakavyo na ukayafurahia maisha kwa muda mfupi huku unajiandaa na mateso ya muda mrefu.
Nikutakie wakati mwema rafiki,
Kwa siku saba zijazo sitakuwa napatikana kwenye mtandao na pia sitaweza kujibu email na jumbe nyingine. Kwa simu pia nitapatikana kwa nafasi ndogo sana.
Kama utapenda kushiriki semina ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO, ambayo itafanyika kwa njia ya wasap na kupata nafasi ya kupata mafunzo mengine kwa mwaka mzima wa 2017 basi lipa ada yako ambayo ni tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253. Ukishatuma fedha tuma ujumbe wenye majina yako kamili na taarifa zako zitawekwa vizuri kwa ajili ya kuingia kwenye kundi la semina. Kama unataka kweli nafasi ya kushiriki semina hii, basi nakushauri ufanye malipo yako mapema.
Nikutakie sikukuu njema rafiki yangu,
Usherekee kwa amani, upendo na utulivu. Ukumbuke kwamba kuna maisha baada ya sikukuu hizi, hivyo usifanye mambo kwa mkumbo.
Tukutane tarehe 30/12/2016 baada ya kumaliza likizo yangu. Nitakushirikisha mengi nitakayotoka nayo kwenye likizo hii.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.