Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Hii ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tunachofanya.

img-20161217-wa0002
Muda tulionao leo ni muhimu sana, tuutumie vizuri.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu BOTTLE NECK….
Kwa chupa za kawaida, mdomo wa chupa ni mdogo kuliko chupa yenyewe.
Na hii imekuwa inapelelea kitu chochote kilichopo kwenye chupa kisitoke kwa urahisi.
Yaani ni vigumu kumimina kwa haraka kitu kilichopo ndani ya chupa kutonana na mdomo mdogo wa chupa. Na hivyo mdomo huo mdogo wa chupa ndiyo kikwazo cha mmiminiko kuwa haraka.

Sasa kwenye mfumo wowote huwa kuna eneo ambalo linafanya mwendo wa vitu usiende haraka. Kuna eneo ambapo linapunguza kasi na hivyo kupunguza kasi ya mfumo mzima. Kama ni kiwandano, basi unakuta eneo fulani linakwenda taratibu na hivyo kukwamisha kabisa uzalishaji. Eneo hili linajulikana kama BOTTLENECK.

Kwenye maisha yako pia una eneo kama hilo.
Kuna eneo kwenye maisha yako ambapo mambo yanakwenda taratibu na hii kupelekea maisha yako yote kuwa taratibu.
Asubuhi hii tafakari ni eneo au maeneo gani kwenye maisha yako ambayo yamekuwa yanakwenda taratibu kiasi cha kukuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Yachunguze maisha yako na utaona kwa urahisi kabisa wapi mamno yanapokwama. Jua maeneo hayo na yafanyie kazi ili uweze kwenda vizuri.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki yako
#KochaMakirita