Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu ambapo tunakwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupata matokeo bora zaidi.

img-20161217-wa0002
Tutumie nafasi hii ya leo vizuri rafiki ili tuweze kufanya makubwa.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTOROKA….
Mara nyingi tumekuwa tunatoroka hali fulani ambazo hatuzitaki kwenye maisha yetu.
Pale tunapojikuta kwenye matatizo au changamoto, tunatoroka ili tusiendelee kuumizwa na hali hizo.
Hasara ya kutoroka ni kwamba haitusaidii chochote, zaidi ya kusogeza matatizo hayo mbele, na kuyaacha yakue zaidi kiasi cha sisi kushindwa kuyatatua.

Ni njia zipi ambazo tumekuwa tunatumia kutoroka matatizo na changamoto zetu?
Zipo njia nyingi, baadhi ni hizi;
1. Kutumia vilevi.
2. Kufuatilia mambo ya wengine.
3. Kuangalia tv.
4. Kusoma gazeti au hata kitabu.
5. Kuamua kujisahaulisha, kama vile kitu hicho hakipo.

Tufanye nini?
Tujikamate pale tunapotaka kutoroka, na kujilazimisha kukaa na hali ile inayotusumbua mpaka tutakapoitatua.
Tukae na changamoto tuliyonayo, na kuitafutia ufumbuzi mpaka tupate njia bora ya kuchukua.
Tunapitamani kutoroka, basi tujikamate na kutudi pale kwenye changamoto mpaka tutakapoitatua.

Njia bora ya kutatua matatizo yoyote au kuvuka changamoto yoyote ni kuitatua na siyo kuitoroka.
USITOROKE

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
Contacts; +255 717 396 253 / makirita@kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.