Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA kwenye kila tunachofanya kwenye maisha yetu, ili kuweza kupata matokeo bora.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kufanya mabadiliko madogo leo.
Kama ambavyo tunajua, mafanikio kwenye maisha hayatokei kama ajali, kwamba ghafla kila kitu kinakuwa vizuri.
Badala yake mafanikio ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo yaliyofanywa kwa muda mrefu.
Hivyo basi, leo tunajukumu la kwenda kubadili kitu leo.
Katika kazi au biashara tunazofanya, tuangalie eneo ambalo tunaweza kulibadili leo. Tuangalie kitu kidogo ambacho tunaweza kukifanya kwa ubora zaidi. Tunaweza kukiboresha zaidi kwa kubadili namna tunavyokifanya.
Kwa kuanza hivi leo, na kuendelea kufanya hivi kila siku, tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kufanya makubwa kadiri tunavyoendelea.
Usisubiri siku moja mambo yabadilike, bali badili mambo kila siku na baada ya muda utajikuta upo kwenye nafasi nzuri zaidi.
Wakati wa kuchukua hatua ni sasa, leo hii, hapo ulipo.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Nenda ukajitume, ushinde na kushukuru.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.