Asubuhi njema rafiki,
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo ambapo tunapata nafasi nyingine ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tunafanya.

IMG_20170102_073855
Tutumie nafasi ya leo vizuri ili tuweze kufanya makubwa.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu takwimu.
Zipo takwimu nyingi mno kwenye maisha ya kawaida.
Mfano wa takwimu ni kama ifuatavyo;
Asilimia 80 ya biashara zinazoanzishwa zinakufa ndani ya miaka mitano.
Asilimia 90 ya watu ni masikini ambao hawana uhakika uhuru wa kipato.
Asilimia 50 ya ndoa zinavunjika.
Asilimia 80 ya watu hawapendi kazi wanazofanya.
Na nyingine nyingi.
Zipo takwimu nyingi mno kwenye kila eneo la maisha, kuanzia afya, kazi, biashara, mafanikio.

Ninachotaka kukuambia asubuhi ya leo ni usiwe takwimu.
Usikubali kuwa sehemu ya hao ambao ni wengi, ambao maisha yao ni magumu kutokana na namna walivyochagua.
Kataa kuwa takwimu
Kataa kuwa upande wa wanaopoteza,
Na chagua maisha ya mafanikio,
Pigana kwa kila hatua mpaka ufikie yale maisha ya ndoto zao.
Ukizembea utaishia kukamilisha yakwimu, na hakuna zaidi ya hapo.
Kama asilimia 80 ya biashara zinakufa, safi, wewe kuwa kwenye ile asilimia 20 ambayo biashara hazifi.
Kama asilimia 90 ni masikini wasiokuwa na uhakika wa kipato, basi wewe kuwa kwenye ile asilimia 10 ya wenye uhakika wa kipato.
Inawezekana ukishaamua iwezekane na kukataa kuwa sehemu ya takwimu, sehemu ile mbaya, ambapo ndipo wengi walipo.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT