Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

IMG_20170102_073855
Tufanye hivi kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA

Asubuhi ya leo tutafakati kuhusu maamuzi mabovu.
Baadhi ya watu wamekuwa wakiacha kufanya mmamuzi kwa kuogopa kufanya maamuzi mabovu.
Kwa sababu hiyo wanajikuta hawafanyi maamuzi na hivyo kushindwa kuchukua hatua.
Asubuhi ya leo nataka nikukumbushe kwamba maamuzi mabovu ni sehemu ya maamuzi.
Kufanya maamuzi mabovu kunakupa nafasi ya kujifunza na kuboresha zaidi.
Lakini kutokufanya maamuzi kabisa unaendelea kubaki pale ulipo sasa.
Na kwa dunia ya sasa, kubaki pale ulipo ni kuchagua kurudi nyuma,
Kwa sababu dunia inakwenda mbele kwa kasi ya ajabu.

Fanya maamuzi hata kama huna uhakika wa maamuzi unayofanya.
Yakiwa mazuri utapata unachotaka,
Yakiwa mabaya utajifunza na angalau utakuwa umechukua hatua.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz