Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunaweza kufanya mambo makubwa aana.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu vitu vidogo visivyodhibitiwa.
Mambo yote makubwa huwa yanaanza madogo,
Hata mbuyu ulianza kama mchicha,
Matatizo yote makubwa yalianza kama matatizo madogo sana.
Ila hayakudhibitiwa, na baadaye yakakua sana, mpaka kufikia hatua ya kuwa hatatishi.
Kama upo kwenye madeni ya mamilioni sasa, hukuanza na mamilioni, bali ulianza kidogo sana, ulianza na maelfu ukashindwa kudhibiti na yamefika mamilioni.
Kama una tatizo la kukosa maelewano mazuri na watu wa karibu hilo pia lilianza kidogo, mkashindwa kudhibiti na hatimaye limekuwa kubwa zaidi.
Chochote kile ambacho ni kikubwa na kinakusumbua sasa hivi, kilianza kikiwa kidogo sana.
Hivyo rafiki yangu, leo na kila siku, angalia ni mambo gani madogo sasa ambayo usipoyachukulia hatua yatakuja kuwa makubwa na yakusumbue sana.
Angalia kwenye kazi, biashara, fedha, afya na hata mahusiano.
Usiruhusu tena jambo lolote dogo lije kuwa kubwa na kukusumbua.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz