Habari za keo rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo ambapo tuna nafasi kubwa ya kwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupata matokeo bora.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao tuna uhakika wa kufanya makubwa kwenye siku yetu hii nzuri sana ya leo.

IMG_20170102_073855

Leo tutafakari kuhusu KUAHIDI MAKUBWA NA KUTIMIZA.
Kwa miaka mingi, dhana kuu kwenye kazi na hata biashara ni AHIDI KIDOGO NA TIMIZA MAKUBWA (UNDER PROMISE AND OVERDELIVER ).
Dhana hii ilifanya kazi siku za nyuma, lakini kama unavyojua, mambo yanabadilika.
Sasa hivi huwezi tena kuwaahidi watu kidogo ili wakikupa nafasi utimize makubwa.
Kwa sababu wakati wewe unaahidi madogo, wenzako wanaahidi makubwa na wanayatimiza. Hakuna mtu mwenye akili zake timamu ambaye atakuja kwenye ahadi kidogo wakati kuna ambaye anaahidi makubwa na upo ushahidi wa yeye kuweza kuyatimiza.
Hivyo, kuanzia leo, mambo yote ambayo yapo ndani ya uwezo wako, kwenye kazi na hata biashara, AHIDI MAKUBWA SANA, halafu pambana mpaka uyatimize.
Hii ndiyo nafasi pekee ya kupona kwenye soko la sasa ambalo mteja ana nguvu kubwa mno kuliko muuzaji.

Dhana hii ina madhara makubwa sana kwako na shughuli zako pale utakapiahidi makubwa na ukashindwa kuyatimiza.
Yaani njia ya haraka ya kuchafua jina lako na kuharibu biashara yako ni kuahidi mambo ambayo huwezi kuyatekeleza.
Hivyo hakikisha chochote unachoahidi, unakitekeleza, kama uliyoahidi, na tena uende hatua ya mbali zaidi.
Tumia kila ulichonacho kuhakikisha unatimiza kila ulichoahidi, jina lako lisije kuwa la mtu anayeongea sana lakini matendo sifuri.

Kwa kifupi, badala ya UNDERPROMISE AND OVERDELIVER unachopaswa kufanya ni ku OVERPROMISE AND OVERDELIVER. Mfanye mtu aone kama amekuibia, kwa namna unavyompa thamani kubwa, ambayo hakutegemea kuipata na hajawahi kuipata kwingine.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT