Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Hii ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile ambacho umechagua kufanya.

Kumbuka leo ndiyo leo, jana ulijiahidi leo, hivyo basi, heshimu maamuzi yako na fanya kile ambacho ulijiahidi kufanya leo. Leo hii tunaongozwa na NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA katika kuhakikisha tunafanya makubwa.
Asubuhi ya leo tutafakari kubusu maamuzi bora,
Kuna watu ambao wanaonekana kuweza kufanya maamuzi bora sana.
Wao kila wanachofanya kinaleta matokeo mazuri mpaka unaweza kuona wao walizaliwa na uwezo mkubwa wa kufanya mamuzi.
Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye anazaliwa akiwa na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi. Kila kitu kinatengenezwa na hata uwezo wa kufanya maamuzi bora pia unatengenezwa.
Kwa kifupi ni kwamba;
MAAMUZI NI MATOKEO YA UZOEFU,
NA UZOEFU NI MATOKEO YA MAAMUZI MABOVU.
Hivyo basi rafiki yangu, huwezi kufanya maamuzi bora kabla hujapata uzoefu wa kufanya maamuzi mabovu.
Ndiyo maana baadhi ya watu wamekuwa wanasisitiza mtu ushindwe haraka ili uweze kufanikiwa haraka. Kwa sababu kushindwa hakuondolewi moja kwa moja, unaposhindwa unajifunza ili usirudie tena makosa.
Hivyo kama unataka kuweza kuwa na maamuzi mazuri, anza kufanya maamuzi yoyote, na kama ni mabovu utajifunza kwa kile utakachopoteza.
Hasara kubwa ipo kwa wale ambao wanafanya mmauzi mabovu na bado hawajifunzi. Wanapopata matokeo mabaya wanajidanganya kwa kutafuta watu wengine wa kuwalaumu.
Jifunze kwa kila unachofanya, kila maamuzi unayofanya kipo cha kujifunza. Jifunze na uchukue hatua, usirudie kitu kilichokuletea hasara.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.