Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.

Tutumie siku hii ya leo kufanya makubwa kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UBISHI…
Hakuna chochote kikubwa unachotaka kwenye maisha yako ambacho kitakuja kirahisi.
Haitatokea hata mara moja kila kitu kikaenda kama ulivyopanga.
Kila wakati zitatokea changamoto za kukuzuia kupata kile unachotaka.
Kuna wakati utaona kama haiwezekani yena kufika kule unakotaka, hasa unapokutana na changamoto ambayo ni kubwa sana.
Ni hatua hii ambapo wengi huishia na kushindwa kupiga hatua, na kukubaki kubaki pale walipo.
Wanakubali kwamba mafanikio ni magumu na hayawezekani.
Lakini wewe mwanamafanikio hupaswi hata kufikiri kwamba changamoto unazokutana nazo ni mwisho.
Unahitaji kuwa mbishi, unakutana na changamoto lakini unazigomea, hukubali ziwe ndiyo mwisho wa safari yako.
Kwa sababu unajua changamoto ndizo zinazokufikisha kule unakotaka kwenda.
Unapozivuka changamoto unakuwa umejifunza zaidi na kupata mbinu za kuwa bora sana.
Ukishajua unachotaka hasa ni nini,
Ukishaiona ndoto kubwa ya maisha yako,
Weka juhudi kuifikia,
Usikubali chochote kikurudishe nyuma,
Kuwa mbishi, wabishi ndiyo wanaofanikiwa.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.