Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi nyingine nzuri sana ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile ambacho tumechagua kufanya.

IMG_20170102_073855

Msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ndiyo utatufikisha mbali zaidi kwa kutuwezesha kufanya makubwa zaidi.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu ACTION na REACTION.

Kuna watu wanafanya jambo kwa sababu wamepanga kulifanya na kwa sababu ni muhimu kwao, lina mchango kwa kule wanakoelekea, hii ni ACTION.
Ukiwa mtu wa action, unapanga kila unachotaka kufanya na utakifanya muda gani ili uweze kufikia ndoto kubwa ya maisha yako.
Action ni muhimu mno kuweza kupiga hatua.

Wapo watu ambao hawawezi kufanya vitu vyao wenyewe, bali wanasubiri wengine wafanye halafu ndipo na wao wafanye kwa kuwaiga au kuwapinga, hii inaitwa REACTION.
Kwa kuishi kwenye reaction unakuwa huna ndoto yoyote kubwa, unasubiri watu wafanye ndipo na wewe ufanye, hakuna unachopigania bali unaendeshwa na matukio ya wengine.
Wanaoishi kwa reaction huwa hawafiki mbali, kwa sababu watakachofanya kesho kinategemea na wengine wanafanya nini.

Hatari kubwa ni kwamba sasa hivi wengi wanalazimishwa kuishi kwa REACTION, hasa uwepo wa mitandao ya kijamii na habari zisizokauka.
Wengi wamekuwa wanazianza siku zao kwa kuREACT na habari mbalimbali za siku hiyo au yale wengine wanayofanya.

Nitachotaka kukuambia rafiki yangu ni hichi, acha kuishi kwenye reaction, anza kuishi kwenye action.
Kila unachofanya hakikisha umepanga kukifanya na kina mchango kufikia ndoto zako kubwa. Usikazane tu kufanya kwa sababu kila mtu anafanya. Wewe pakee ndiye balozi wa ndoto zako, hivyo kazana uweze kuziishi. Acha wengine nao wakazane na ndoto zao.
Usishindane na wengine,
Usitake kuwaonesha wengine kwamba wewe upo sahihi zaidi,
Usitake kufanya ili kuonekana na weee upo,
Bali fanya kwa sababu inakupeleka kwenye ndoto zako kubwa.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.