Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora zaidi.

IMG_20170102_073855
Leo hii ishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili uweze kufanya makubwa zaidi.

Asubuhi ya leo tutafakari unachojulikana nacho,
Je ni sifa gani unayo mbele ya wengine?
Jina lako linapotajwa, watu wanafikiria nini?
Watu wanaipa sifa gani kazi au biashara unayofanya?
Wanakichukuliaje kile ambacho unafanya kwao?

Najua huwezi kuchagua au kulazimisha watu wajisikieje juu yako, lakini kujua hili kunaweza kukupa taswira ya wapi unaelekea.
Siri kuu ya mafanikio ni kuwa vizuri kwenye kitu fulani,
Kuchagua kitu ambacho utakuwa bora sana,
Na kuweka juhudi zako zote kuhakikisha unakuwa bora.

Hivyo tafakari yako ya leo, itakupa mwanga iwapo watu wanakuchukulia kwa ile namna ambayo umechagua kuwa bora sana.
Chagua unataka kuwa bora kwenye nini, chagua maisha yako unataka yaguseje maisha ya wengine, kisha fanyia kazi hilo, KILA SIKU.
Kuwa bora leo zaidi ya ulivyokuwa jana.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.