Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni zawadi ya kipekee sana kwetu kwenda kufanya makubwa siku ya leo.
Ni jambo la kushukuru kuiona siku hii kwa sababu wapo wengi walioipangilia kabisa siku ya leo, lakini hawajaweza kuiona, au hawataweza kuifanyia kazi kama walivyopanga, kutokana na sababu mbalimbali.

IMG_20170102_073855
Wewe uliyepata nafasi hii, itumie vizuri sana, usiseme tena utafanya kesho, kwa sababu huna uhakika na hiyo kesho.
Leo tunakwenda kuongozwa na msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na tutaweza kufanya makubwa sana.
Pia tutaweza KUTHUBUTU, KUSHINDA NA KUSHUKURU kwa kila tutakachopata siku ya leo.

Asubuhi ya leo hebu tutafakari hazina muhimu sana kwenye maisha yetu.
Nianze hivi, muda wetu hapa duniani ni mfupi sana, ukilinganisha na umri ambao dunia imekuwepo na itaendelea kuwepo.
Ukilinganisha miaka bilioni ya dunia, na miaka 100 ambayo unaweza kuishi, 100 ni namba ndogo mno.
Pia makosa ya kufanya ni mengi, lakini muda na nguvu ya kuyafanya yote huna. Si unajua faidanya makosa, ambayo ni kujifunza zaidi.
Tunahitaji kuwa na maisha mengi zaidi ndani ya muda mfupi tutakaoishi, na pia tunahitaji kujifunza zaidi ndani ya muda huu.
Ipo njia ya mkato ya kufikia hilo, njia hiyo ni KUSOMA VITABU.

Kusoma vitabu ni hazina kuhimu sana.
Ukisoma vitabu vilivyoandikwa miaka 2000 iliyopita, unakuwa umeishi maisha mengi ndani ya muda wako mfupi. Unakuwa umeweza kutembelea maisha ya wengine na kujifunza.
Pia kupitia vitabu, unaweza kujifunza kutokana na makosa ya wengine, hivyo huhitaji kurudia tena makosa yao.
Vitabu ni hazina kubwa sana, na kwa zama hizi, vipo vitabu vya kitu chochote unachotaka kujifunza.

Swali ni je unasoma vitabu?
Umeshasoma vitabu vingapi mpaka sasa kwa mwaka huu 2017 pekee.
Kama husomi, jua kabisa umechangua njia ya kupotea.

Uwenna siku njema rafiki.
Kwa vitabu tembelea http://www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,