Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nzuri sana ya leo.

Ni matumaini yangu umeianza siku hii vyema na upo tayari kwenda kuweka juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa.
Nafasinya leo ni ya kipekee, itumie vizuri.
Kumbuka msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao ndiyo unaotuwezesha kufanya makubwa.
☕☕Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu OPTIONS yaani MACHAGUO.
Uhuru wako kwenye maisha ni pale unapokuwa na option nyingi, yaani unapokuwa na uwezo wa kuchagua kati ya vitu vingi, ndivyo unavyozidi kuwa huru.
Na hiki ndiyo kitu kikuu ambacho uhuru wa kifedha unaleta kwenye maisha yako, kuweza kuchagua kadiri utakavyo.
Kukosa nafasi hii ya kuchagua kile unachotaka, kumesababisha watu kuishi kwenye ufungwa, kuishi maisha ambayo hayana uhuru na kufanya mambo ambayo hawapendi kufanya.
Swali ni je, ni machaguo mangapi unahitaji kuwa nayo ili angalau uanze kuwa na uhuru?
1⃣Ukiwa na chaguo moja, huna chaguo, yaani huna namna. Ni sawa na pale ambapo chanzo chako cha kipato ni mshahara pekee, na ndiyo unautegemea kwa kila kitu, huna uchaguzi, mwajiri wako akikuambia nakuondoa hapa ulipo na kukupeleka mkoa mwingine, huna uchaguzi, itakubidi ufanye, hata kama hupendi. Ndiyo ubaya wa kuwa na chaguo moja pekee.
2⃣Ukiwa na machaguo mawili unakuwa na mtaziko (dilemmma), hapo sasa ndiyo mambo yanakuwa magumu zaidi, hujui ufanye A au ufanye B. Kila moja inaonenaka sahihi na muhimu kufanya. Unaweza kuchukua muda mwingi kufikiria ipi sahihi kufanya kati ha hayo mawili. Hapa pia huna uhuru, na unajitesa zaidi kufikiri ipi bora.
3⃣Ukiwa na machaguo matatu, hapo saaa unaweza kuchagua, unaweza kuangalia kila moja, faida na hasara na kuamua kwenda na changuo moja. Hapa ndipo unapoweza kuchagua kipi upo tayari kufanya na kusimamia.
Hivyo rafiki, kwenye kila kitu cha maisha yako, hakikisha una machaguo mengi.
💵 Na hili lianzie kwenye kipato, usiwe na chanzo kimoja pekee cha kipato, hata kama ni biashara, isiwe moja tu. Hakikisha unajijengea vyanzo vingi vya kipato, ili kuongeza uhuru wako wa kifedha.
Kwa mambo mengine, ukishakuwa na uhuru wa kifedha, unakuwa na nguvu kubwa ya kuchagua.
Tengeneza options nyingi kwenye maisha yako.
Nakutakia siku njema sana ya leorafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.