Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Ni imani yangu kwamba umeianza siku ya leo vizuri.
Hii ni siku nyingine bora sana kwetu ambapo tunapata nafasi ya kwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupata matokeo bora zaidi.
Tukitumia vizuri muda wetu wa leo, tutapiga hatua kubwa kukaribia ndoto zetu.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu FIRE ON ALL CYLINDERS…
Mashine zote ambazo zimewahi kutengenezwa hapa duniani, zimechukua mfano kwenye mwili wa binadamu.
Ndiyo maana kila mashine inapewa chakula (mafuta) inahitaji hewa ya oksijeni na inatoa moshi wenye kabondayoksaidi.
Kama ambavyo sisi tunakula chakula, tunavuta hewa safi na kutoa hewa chafu.
Chakula kinaunguzwa na hewa safi, kinatoa nguvu na hewa chafu. Nguvu hii ndiyo inatuwezesha kufanya shughuli zetu mbalimbali. Na hata kwa mashine pia, hali ndiyo hiyo hiyo.
Sasa changamoto kubwa ni kwamba, watu wengo hawatumii vizuri mashine kuu na muhimu wanayoimiliki. Wanatumia sehemu kidogo sana ya mashine hii, na hivyo kutokuifaidi vizuri.
Yaani ni sawa na mtu mwenye gari yenye uwezo wa kubeba tani kumi, anabeba nayo kilo 10 za mchanga na kuendesha kwa kasi ya kilomita 5 kwa saa. Ni matumizi ya chini kabisa ya uwezo mkubwa wa gari hiyo.
Hivyo rafiki yangu, utumie mwili wako vizuri, nasema FIRE ON ALL CYLINDERS.
Miili yetu ni sawa na ina CYLINDER 10 lakini sisi tunatumia moja tu.
Ninachotaka kusema ni kwamba, una uwezo wa kufanya makubwa kuliko unavyofanya sasa. Na ili uweze kufanya hayo makubwa, lazima ubadili namna unavyofanya.
Lazima uweze kutumia mwili wako vizuri, lazima uweze kuvuna nguvu za mwili wako katika kufanya makubwa.
Ili uweze kutumia vizuri nguvu za mwili wako na kufanya makubwa, kwanza jua una nguvu kiasi gani, na hapa unahitaji kuweka juhudi zaidi mpaka pale unapoona huwezi kuendelea tena.
Mara nyingi watu wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea, hivyo hawajui hata ni mbali kiasi gani wanaweza kufika. Anza kujua hilo na weka kazi.
Muhimu; unapofire on all cylinders unahitaji kuifanyia mashine service ya uhakika. Hivyo hakikisha mwili wako upo kwenye hali nzuri wakati wote, ili uweze kuutumia vizuri kufikia mafanikio makubwa.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT