Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Hakikisha siku hii ya leo unaitumia vizuri rafiki, unachoweza kufanya leo kisingoje kesho.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunaweza kufanya makubwa zaidi siku ya leo.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NI MAISHA YAKO….
Wapo watu wengi, ambao wameshindwa kufanya maamuzi muhimu ya maisha yao, kwa kuhofia wengine watawachukuliaje.
Wanafikiria sana namna wengine watakavyowasema na kuwahukumu, au kuwadharau na kuwakatisha tamaa.
Kwa namna hii mtu anaona ni bora asifanye maamuzi fulani.

Kwa kuchukua hatua hii, mtu anafikiri amewaridhisha watu, lakini anasahau kwamba amejinyima mambo muhimu sana kwenye maisha yake. Kila siku atakuwa akijiambia, ningeweza hili au lile, lakini hafanyi.

Ninachotaka uondoke nacho asubuhi ya leo rafiki ni kwamba hayo uliyonayo sasa ni maisha yako. Hakuna mtu mwingine yeyote atakayeishi maisha hayo ila wewe binafsi. Hivyo usiogooe kufanya maamuzi kwa sababu unahofia wengine watakuchukuliaje.
Hakuna anayeweza kujali maisha yako zaidi yako binafsi.
Yape maisha yako kipaumbele na siyo mitazamo ya wengine.
Chochote muhimu kwako kufanys, fanya.
Wengine hata hawajali sana kuhusu maisha yako, maana maisha yao yenyewe yanawapa changamoto kubwa.

NI MAISHA YAKO, NI WAJIBU WAKO KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NA MUHIMU.

Uwe na siku bora na ya kipekee sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.