Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

Tukumbuke kwamba maisha yetu ni jukumu letu, hivyo lazima tuchukue hatua.
NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ni msingi muhimu kwetu kuwa na mafanikio makubwa.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu BLIND SPOT…
Japokuwa jicho lako unaliamini, jicho lako linakuonesha kila kitu unachotaka kuona, ipo sehemu kwenye jicho lako haioni kabisa. Yaani haioni chochote kwa sababu imekosa zile seli zinazohusika na kuona. Sehemu hii inaitwa BLIND SPOT. Ni kaeneo ambapo una upofu.
Tatizo la blind spot ni kwamba wewe mwenyewe huwezi kujua kama kuna sehemu huoni, hivyo unaona kila kitu kipo poa kabisa.
Kwenye kazi zetu, biashara na hata maisha kwa ujumla, kuna maeneo ambayo ni BLIND SPOT Kwetu. Maeneo ambayo hatuyaoni kwa uhalisia wake. Sisi tunadhani yapo poa kabisa kumbe siyo. Tunaona tunafanya vizuri kabisa kumbe tunakosea.
Hapa ndiyo muhimu sana kupokea na kufanyia kazi maoni ya wengine. Uzuri ni kwamba pale ambapo hatupaoni sisi, wengine wanapaona vizuri. Hivyo wanaweza kuwa na maoni na mchango kwenye kile tunachofanya na namna tunavyofanya.
Hivyo unahitaji kusikiliza mrejesho na maoni kwa wale ambao wanapokea au kuathirika na kile unachofanya. Hawa watakuonesha pale ambapo wewe huoni ili uweze kuchukua hatua.
Hakikisha upofu wako haukupotezi, wapo wengi wanaoona pale ambapo huoni wewe, sikiliza na fanyia kazi yale wanayokushauri.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.