Kumekuwepo na mifumo mbalimbali ya falsafa tangu kuwepo kwa dunia.
Kwa sababu mara zote watu wamekuwa wakihoji juu ya mambo mbalimbali, kama uwepo wa dunia na mengine.

Falsafa ilikuwa ikichukuliwa kama kitu cha kufikiria na kubishana pekee. Mpaka wakati wa mwanafalsafa Socrates, ambaye hakuishia tu kufikiri na kuhoji, bali alifanya falsafa kuwa sehemu ya maisha yake, aliishi kila siku kwa falsafa.
Aliwafundisha watu namna ya kuishi kwa falsafa, kitu kilichompelekea ahukumiwe kujiua kwa tuhuma za kuwaharibi vijana.

Baada ya socrates zilifunguliwa shule mbalimbali za falsafa, ambapo wazazi walipeleka watoto wao wakajifunze falsafa. Zilikuwepo shule nyingi, na moja ya shule hizi ni USTOA, ambapo watu hawakuishia tu kujifunza, bali waliishi falsafa zao.

Ni aibu kwa sasa hakuna shule za falsafs, shule ambapo mtu anaweza kwenda na kujifunza falsafa ya maisha. Mtu anaweza kujifunza falsafa kwenye elimu ya chuo kikuu, lakini ni kwa sababu tu ya kupata cheti, yaani kuhitimu masomo yake, na labda baadaye kupata kazi.
Kupata shule ya falsafa, inayofundisha namna ya kuwa na maisha bora, ni vigumu.

Mtu anaweza kwenda kwa kiongozi wake wa dini, lakini yeye atamwambia namna ya kuwa mtu mzuri, kwa kuwajali wengine na kutokutenda dhambi, ja namba ya kufika mbinguni kwa kusali sana na kutoa sadaka. Lakini namna ya kuwa na maisha bora na yenye furaha, hawezi kupata jibu hilo.

Hilo ndiyo jibu tunalokwenda kupata kwa kujifunza falsafa ya ustoa.
Karibuni tuendelee kujifunza falsafa hii muhimu kwetu na kuweza kuiishi ili kuwa na maisha bora na yenye furaha.