Mambo muhimu niliyojifunza kwenye utangulizi wa kitabu A GUIDE TO GOOD LIFE.
Hichi ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi na mwanafalsafa Willium ambaye alikuwa akitafiti kuhusu Tamaa.
Baada ya kuangalia dini zinasemaje kuhus tamaa, hakupata maarifa ya kutosha, ndipo alipogeukia falsafa na kukutana na falsafa ya ustoa, ambayo imeelezea kwa kina sana kuhusu tamaa na hisia nyingine za binadamu.

Watu wengi wanaishi maisha yao, wakiwa hawajui lipi hasa lengo kuu la maisha yao. Wanasukuma siku wakiwa hawajui kipi hasa wanachotaka. Wanaishia kupoteza maisha na kukosa kuridhika na maisha yao.

Watu wengi wanaojifunza falsafa ni kwa ajili tu ya kupata cheti cha elimu, lakini siyo kwa ajili ya kuishi falsafa hiyo.
Falsafa ya ustoa, ni moja ya falsafs muhimu ambazo ukiishi unakuwa na maisha bora.

Watu wengi wamekuwa wanachukulia wastoa kama watu ambao hawana hisia au wanakandamiza hisia zao, lakini huo siyo ukweli, wastoa ni watu ambao wanaweza kudhibiti hisia zao na siyo kuruhusu hisia ziwaendeshe.

Wastoa wa zamani walikuwa na maisha tofauti na falsafa, wapo waliokuwa waandishi na matajiri kama Seneca, wengine walikuwa wakosoaji wa serikali kama Cato, na pia walikuwepo watawala kama Marcus Aurelius.

Falsafa ya ustoa haiingiliani na dini yoyote, yaani haipingani na dini yoyote. Ukiangalia dini kama ukristo, inaendana kwa kiasi kikubwa na falsafs ya ustoa.

Kuiishi falsafa ya ustoa ni kazi, lakini pia kuishi bila falsafa ni kazi, hivyo bi vyema kuchagua falsafa ya ustoa ambayo itakupa maisha ya maana kuliko kutokuwa na falsafa kabisa.

Kupitia kitabu hichi, tutajifunza kwa kina kuhusu falsafa hii na namba ya kuiishi ili kuwa na maisba bora.

Asanteni.

 

Unaweza kupakua na kusoma kitabu hichi hapa;

A Guide to the Good Life The Ancient Art of Stoic Joy – William Braxton Irvine