Kama lipo swali gumu kwa mtu yeyote kujibu basi ni hili; lipi kusudi la maisha yako? Upo hapa duniani kufanya nini?
Ni swali gumu sana kujibu kwa sababu kuu moja, ulipozaliwa, hukuja na kijitabu cha maelezo kwamba umekuja na uwezo gani na utaweza kufanya mambo gani vizuri. Kwa kifupi ulikuja hapa duniani watu wakiwa hawaelezi una uwezo gani na vipaji gani.
Kwa bahati mbaya sana, ukaingia kwenye jamii ambayo ilikuwa inaamini kitu kimoja tu, kwamba ili uwe na maisha mazuri, basi lazima usomee taaluma nzuri kama udaktari, ualimu, sheria, uhasibu na nyingine za aina hiyo na upate ajira.
Hivyo vile viashiria vya kusudi la maisha yako vilipokuwa vinajitokeza kwako, vilizimwa haraka sana kama vilikuwa vinakwenda kinyume na matarajio ya jamii. Kwa mfano ikiwa ulikuwa unapenda sana kucheza mpira, huenda wazazi wako walikuambia achana na huo mpira, hauwezi kukulipa, kazana na masomo ufaulu vizuri ili uwe na kazi nzuri.
Au ulikuwa unapenda sana kuimba na wakakuambia kuimba ni uhuni tu, hakuna kikubwa unachoweza kupata.
Na wakati mwingine, pale ambapo umekazana kujitoa kwenye huo mtego, labda ukakwepa kuajiriwa licha ya kusoma vizuri, ukawa umeshaanza kujua kipi hasa unapenda kufanya na ukaanza kufanya, jamii itaanza kukuangalia kwa jicho la tofauti, na siyo jicho zuri. Wapo watakaokuuliza lini utapata kazi ya maana? Wengine wataona umechanganyikiwa au hujui unachotaka na unachofanya.
Kwa mazingira haya na mengine mengi ambayo sijaeleza hapa, kujua kusudi la maisha yako na kuweza kulitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako, ni kitu kigumu sana na unakwenda kinyume na jamii nzima inayokuzunguka. Ndiyo maana ni wachache sana ambao wameweza kujua kusudi la maisha yao na kuweza kulitumia.
Ninachotaka kwako rafiki yangu ni wewe pia ujue kusudi la maisha yako na uweze kulitumia, kwa sababu, bila ya kulijua maisha yako hayawezi kukamilika, hata kama ungekuwa na fedha nyingi kiasi gani.
Kama umewahi kusikia watu wanasema wapo matajiri wenye fedha nyingi lakini hawana furaha, basi chanzo ndiyo hicho, walikazana kutafuta fedha, wakalisahau kusudi la maisha yako.
Kwenye somo letu la leo la ONGEA NA COACH, nimekushirikisha namna unavyoweza kujua kusudi la maisha yako na kulitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Angalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya.
Kama kifaa chako kinaruhusu unaweza kuliangalia hapo chini.
Kwa kupata masomo zaidi bonyeza maandishi haya, utajifunza mengi sana kwa masomo ya video.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.