Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

IMG_20170102_073855
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa.

Asubuhi ya leo tunatafakari kuhusu NO GUARANTEE.
Tunapokwenda kununua vitu, tunapenda sana vile vitu ambavyo vina guarantee, kwamba tuna unakika vitafanya kile tunachotaka, na kama itakuwa tofauti basi tunaweza kurudisha tuliponunua.

Sasa wengi wamekuwa wakifikiri maisha pia yapo hivyo.
Kwamba ukishafanya kile unachopaswa kufanya, basi umejihakikishia kupata kile unachotaka kupata.
Lakini maisha hayaemdi hivyo.
Unaweza kufanya kila unachopaswa kufanya lakini usipate kile unachotaka kupata.

Hakuna guarantee yoyote, unaweza upate au usipate.
Lakini hii haipaswi kukukatisha tamaa.
Kwa sababu ukifanya unachopaswa kufanya, unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupata unachotaka.
Lakini usipofanya kabisa, huwezi kabisa kupata.

Hivyo endelea kufanya, na usipopata unachotaka usikate tamaa, endelea kufanya.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.