Siri Tatu (03) Muhimu Kuhusu Fedha Ambazo Matajiri Wanazijua Lakini Masikini Hawazijui.

Rafiki,
Kama yupo mtu ambaye anapata matokeo tofauti na unayopata wewe, basi kipo kitu anachofanya tofauti na unavyofanya wewe. Hivyo badala ya kujiuliza wao wanawezaje na wewe umeshindwaje, jiulize kipi wanafanya ambacho wewe hufanyi. Ukijua hicho utakuwa umetatua nusu ya tatizo lako.

Changamoto kubwa ni kwamba watu wengi huwa hawakubali kwamba kuna mahali wanakosea, au kukubali kwamba kuna vitu hawajui, wao hukazana kufanya kile walichozoea kufanya na hivyo kuishia kupata matokeo yale waliyozoea kupata.

Sasa turudi kwenye FEDHA, ambayo ndiyo mada yetu ya leo. Kwanza wapo watu watajisikia vibaya tu kwa sababu leo naongelea kuhusu fedha. Hawa ni watu waliokuzwa kwa kuamini kwamba mtu yeyote anayezungumzia fedha ni mtu mwenye tamaa ya fedha na asiyejali wengine. Hivyo watu hao hawazungumzii fedha popote, lakini mawazo yao mengi yapo kwenye fedha, kwa sababu ukiwachunguza, fedha zinawapa shida sana.

Leo nakwenda kukushirikisha siri tatu muhimu sana kuhusu fedha, ambazo matajiri wanazijua na kuzitumia, lakini masikini hawazijui. Ni siri ambazo ziko wazi sana, lakini kwa kuwa masikini hawapendi kuongelea kuhusu fedha, wala kuwasikiliza wanaoongelea fedha, basi wanakosa maarifa haya muhimu.
Nina imani utakwenda kunisikiliza ujue siri hizi tatu muhimu na namna ya kuzifanyia kazi kwenye maisha yako ili uweze kufikia uhuru wa kifedha.

Kwenye video ya somo la leo, nimechambua kwa kina siri hizi tatu muhimu kuhusu fedha, nimeeleza kwa mifano namna unavyoweza kutumia siri hizo ili kuweza kufikia utajiri.
Utajiri, kwa namna ambavyo huwa nasema mimi, siyo lazima uwe na mali nyingi kupita wote, bali wewe ni tajiri pale ambapo fedha inakufanyia kazi wewe. Yaani kama fedha inaingia hata kama hufanyi kazi moja kwa moja basi hapo umeingia kwenye utajiri.
Na umasikini ni pale ambapo unaifanyia kazi fedha, yaani ili upate fedha lazima ufanye kazi moja kwa moja. Haijalishi unapata kiasi gani, hata kama unapewa milioni 10, bado wewe ni masikini kama ukiacha kufanya kazi hiyo huna kipato kinachoingia.

Nisiandike mengi hapa, nakupa muda uangalie somo hili la siri tatu za fedha, angalia, jifunze, zijue na zifanyie kazi kwenye maisha yako. Haihitaji elimu kubwa ili uweze kuzifanyia kazi, ni utayari wa wewe kuchukua hatua ndiyo unahitajika.

Angalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya.

Au pia unaweza kuangalia hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Kwa kuangalia masomo zaidi ya video bonyeza maandishi haya.
Kusikiliza masomo ya sauti bonyeza maandishi haya.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

MUHIMU; KITABU BIASHARA NDANI YA AJIRA PIA KINAPATIKANA HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP ILIYOPO POSTA DAR ES SALAAM, MTAA WA SAMORA, JENGO YA NHC.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: