Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi ya kipekee leo kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.

Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UTAMU NA UCHUNGU…
Utamu na uchungu zote ni ladha, zote ni hali na zote ni hisia.
Moja haiwezi kwenda yenyewe bila mwenzake.
Unapopata utamu pekee, unaanza kuuzoea na kuona ni kitu cha kawaida.
Lakini unapopata uchungu, unakumbuka utamu na namna ulivyo mzuri.
Ukija kupata utamu baada ya kupata uchungu, utauthamini sana utamu ule.
Kwenye maisha huna namna bali kukutana na utamu na uchungu. Katika mengi utakayopitia, utapitia utamu na uchungu, pokea vyote na vitumie vizuri kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora na unapata kile ambacho unakitaka.
Hata kama unapitia uchungu kiasi gani, jua wakati wa utamu unakuja. Hivyo jiandae vyema kwa utamu. Na wakati wa uchungu ndiyo wakati ambao unaweza kufanya makubwa sana, unaweza kubadilika kabisa.
Tumia vizuri utamu na uchungu, maana vyote utakutana navyo.
Mwisho; wapo watu wa aina mbili ambao wanataka utamu tu, hawataki uchungu jata kidogo, wanataka utamu na wanautaka sasa, hawataki kusikia jambo jingine lolote. Watu hawa ni watoto na wapumbavu. Watoto tunajua sababu yao na tunawasamehe, ila wapumbavu, huumia sana kwa kutaka kwao utamu tu.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.