Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa.

img-20161217-wa0002
Tunajua kabisa mafanikio yetu yanatokana na kazi, hivyo lazima tuweke kazi ya uhakika kila siku.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SOLUTION VS DISTRACTION….
Unapokutana na tatizo au changamoto kwenye maisha yako, huwa unachukua hatua gani?
Kwa walio wengi, hatua za kuchukua ni moja kati ya hizi mbili; SOLUTION AU DISTRACTION…

SOLUTION.
Unapochukua hatua ya solution, unachagua kutatua ya kuchukua ili kutatua tatizo au changamoto unayokutana nayo.
Hapa unafanya kile ambacho kitapelekea wewe kuondokana na tatizo lile unalokumbana nalo na kupata kile unachotaka.
Hapa unachukua hatua kubadili mambo.
Na kuchukua hatua ni kugumu, kunahitaji moyo ila kunabadili mambo.

DISTRACTION.
Wengine wanapokutaba na tatizo au changamoto, huamua kujisumbua ili wasione tatizo hilo. Lengo lao ni kukata kwamba tatizo halipo, au kama lipo basi siyo wao wamesababisha au hawawezi kutatua.
Zipo njia nyingi za kukwepa tatizo, wapo ambao wanatumia vilevi wakiamini vitawaondolea shida, wengine wataangalia tv au kuperuzi mitandao ya kijamii kupita kiasi, wapo ambao watalalamika na kulaumu wengine, na wapo ambao watakataa tu kwamba hawana tatizo lolote.
Distraction ni rahisi mwanzoni ila inatengeneza maisha mabovu mno.

Swali langu kwako linarudi tena, unapokutana na tatizo, hatua yako ya kwanza ni ipi? Kuchukua hatua kutatua (SOLUTION ) au kuanza kulalamika na kukimbilia kwenye vilevi na mitandao (DISTRACTION )
Kama unataka maishanya mafanikio, chagua solution muda wote, achana na distraction, haitakufikisha popote.

Usipogeze hata dakika moja kwenye distraction, hakuna faida kabisa.
Hivyo basi, unapokuwa tatizo au changamoto;
Usikimbilie kunywa pombe…
Usikimbilie kuvuta sigara…
Usikimbilie kutumia madawa ya kulevya..
Usikimbilie kulalamika na kulaumu wengine….
Usikimbilie kuperuzi mitandao ya kijamii…
Usikimbilie kuangalia tv,
Bali kaa chini na tatizo lako na jipange unalitatuaje.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.