Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.

IMG_20170102_073855
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo titafakari kuhusu NO MATTER WHAT….
Kupanga kila mtu anaweza kupanga,
Kusema kila mtu anaweza,
Ila inapokuja kwenye utekelezaji, na changamoto kuanza, ndipo mambo hubadilika.
Hapa watu wanakutana na changamoto ambazo zinawarudisha nyuma na kuwafanya wakate tamaa.

Ili kushinda changamoto hizi, lazima ujipe azimio wewe mwenyewe,
Ya kwamba, HAIJALISHI KITATOKEA NINI, LAZIMA UPATE KILE UNACHOTAKA.
Yaani usikubali kabisa chochote kikuzuie wewe kupata kile unachotaka,
Usikubali kusema nimejaribu lakini nimeshindwa,
Jipe azimio la kuhakikisha unapata au unafika unapotaka kufika.

Sasa swali muhimu sana kwako rafiki yangu, ni mambo gani kwenye maisha yako mpaka sasa umeshajiwekea azimio la NO MATTER WHAT…
Kama huna hata moja, maana yake hujui hasa nini unataka, au hujajitoa kweli kupata unachotaka.

Wanasema usipokuwa na cha kusimamia, basi utaangushwa na kila kitu.
Na pia wanasema kama huna kitu ambacho unaweza kukifia, basi hakuna kitu ambacho unaweza kukiishi.
Unahitaji azimio hili la HAIJALISHI KITATOKEA NINI, wewe lazima upate unachotaka na ufike unakotaka.

Weka azimio hili kwenye yale maono yako makubwa na ndoto za maisha yako.
Asitokee mtu yeyote au kitu chochote kukuzuia wewe kuziishi ndoto zako.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.