Kila mwezi nimekuwa nafanya kazi na watu wachache, ambao kuna hatua wamekuwa wanatamani kupiga kwenye maisha yao, lakini wao wenyewe wameshindwa. Wanakuwa wanajua kabisa ni wapi wanataka kufika, lakini wanashindwa kuchukua hatua kutokana na kukosa nidhamu binafsi, au kuwa na sababu nyingi ambazo haziishi.
Nimekuwa nafanya kazi na watu hawa, mmoja mmoja kwa kipindi cha mwezi mmoja, na wengi wamekuwa wanapata matokeo ambayo hawajawahi kuyapata kwenye maisha yao.
Ndani ya mwezi mmoja wanajikuta wanafanya mambo ambayo wamekuwa wanatamani kufanya miaka na miaka lakini hawaanzi.
SOMA; Hizi Ndizo Faida Za Kufunga Ndoa Na Utajiri Na Kuupa Umasikini Talaka.
Sasa nafasi hii inapatikana tena kwa mwezi huu wa tano unaokuja. Zipo nafasi chache sana za coaching kwa mwezi wa tano. Hivyo kama ungependa niwe kocha wako moja kwa moja, kwa kipindi cha mwezi mzima, basi nafasi ndiyo hii.
Katika kipindi hichi cha coaching, tutaweka mipango pamoja ya hatua za kuchukua kila siku ili kuweza kufika pale ambapo unataka kufika. Baada ya hapo unaanza kufanyia kazi na kila siku tunawasiliana huku ukinipa ushahidi wa kipi ambacho umefanya.
Mahitaji ya kujiunga na programu hii ya coaching;
Programu hii siyo kwa kila mtu, hivyo mahitaji muhimu sana ambayo lazima uweze kuyatimiza ili ujiunge na programu hii ni haya;
1. Kuwa na kiu kubwa ya kufanikiwa kwenye jambo fulani unalotaka tufanyie kazi.
2. Kujua ni wapi hasa unakotaka kufika, kama hujui unakokwenda hatuwezi kufanya kazi pamoja.
3. Kuweza kuwasiliana kila siku, na kutoruhusu sababu yoyote ile iingilie mipango tuliyokubaliana kila siku.
Maeneo unayoweza kunufaika na programu hii ya coaching.
Ninaweza kukusaidia sana kwenye maeneo haya yafuatayo;
1. Kujenga tabia mpya za mafanikio.
2. Kuvunja tabia zinazokuzuia kufanikiwa.
3. Kuongeza kipato chako.
4. Kuongeza mauzo kwenye biashara.
5. Kukuza biashara yako.
6. Kujua uwekezaji na kuanza kuwekeza.
7. Kujijengea nidhamu ya fedha na kuondoka kwenye madeni.
8. Kutumia vizuri muda wako na kuongeza uzalishaji.
9. Kuandika kila siku na kuandika kitabu.
10. Kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti.
11. Kujenga tabia ya kusoma kila siku na kusoma vitabu.
Katika hayo unachagua moja au machache (yasiyozidi matatu) na tunayafanyia kazi pamoja.
Ada ya personal coaching ni tsh 100,000/= kwa mwezi. Ni zoezi ambalo litakuwezesha kufanya kile ambacho unaahirisha kufanya kila siku. Nafasi zipo chache sana, watu watano tu ninaoweza kufanya nao kazi kwa mwezi. Hivyo kama utahitaji nafasi hii, tuwasiliane mara moja. Niandikie ujumbe kwa njianya wasap wenye neno PERSONAL COACHING kwenda namba 0717396253. Karibu sana tufanye kazi pamoja.
MUHIMU;
Iwapo utajiunga na program hii ya coaching, na mwisho wa mwezi ukaona hakuna hatua yoyote uliyopiga, licha ya kufanyia kazi yale yote ambayo tumekubaliana, basi unanijulisha program haikuwa na msaada kwako na bila ya kukuhoji neno la ziada, ninakurejeshea ada uliyolipia. Japokuwa naweka muda mwingi kukusaidia, lakini lengo langu kuu siyo kunufaika na ada unayolipa, bali kuhakikisha wewe umepiga hatua.
Karibu sana kwenye programu hii ya coaching, niandikie sasa ujumbe kwa wasap 0717396253 kuwahi nafasi hizi chache.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.
