Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo makubwa sana.

img-20161217-wa0002
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo hakutakuwa na tafakari, bali taarifa.
Na taarifa yenyewe ni kwamba kesho itakuwa mwisho wa #TAFAKARI hizi ambazo nimekuwa nakuletea kila asubuhi.
Kuanzia terehe 01/05/2017 kuna kitu kipya nitakijaribu kwa siku 30, kisha nitafanya tathmini yake na kuona kama nitaendelea nacho au la.

Kitu hicho kinaitwa MONK MODE MORNING.
Monk mode morning ni nini?
Hii ni mbinu ya kuoneza ufanisi ma uzalishaji ambayo inakutaka ujitenge na mambo mengi kwa kipindi kifupi ili akili yako yote iwe sehemu moja.

Hivyo katika hii monk mode morning, kuanzia ninapoamka asubuhi, kwa upande wangu ni saa 10 asubuhi, mpaka saa sita mchana, nakiwa sipatikani kwa namna yoyote ile. Hakuna simu, mesej, intaneti wala email. Huo unakuwa muda wangu wa kuweka kazi kubwa ya siku.
Hivyo nitakuwa nimepata masaa karibu 8 ya kufanya kazi yangu kila siku bila ya usumbufu wowote.
Baada ya saa sita mchana, ndipo sasa naweza kuanza kuruhusu hayo mambo mengine.
Hii ni ngumu kidogo, lakini pia nina imani itaniwezesha kuzalisha kazi nyingi na bora zaidi.

Hivyo kwa kuwa tafakari hizi nilikuwa naziandika live, yaani nikiamka, nafanya meditation kisha naandika makala na baadaye tafakari, sasa sitaweza kufanya hivyo. Kwa sababu kuanzia tarehe moja, sitakuwa online kabla ya saa sita mchana.

Vitu vingine vitabaki kama kwaida, makala za kurasa kila siku kwenye KISIMA CHA MAARIFA zitaendelea kuwepo, hivyo unaweza kuzifuatilia zaidi zikawa mbadala wa tafakari. Pia makala kwenye AMKA MTANZANIA zitaendelea kuwepo, kila siku.
Pia kutakuwa na makala mpya zaidi ambazo zitatokana na njia hii mpya ninayokwenda kutumia.

Niombe radhi kwa wale wote watakaozikosa sana Tafakari, kuna wakati unahitaji kukosa kitu kizuri, ili uweze kupata kilicho bora zaidi.
Tutaendelea kuwa pamoja kila siku, lakini kuwasiliana na mimi kumbukua ni kuanzia saa sita kamili mchana.

Muhimu; kama umeipenda mbinu hii na ungependa kuitumia au kujifunza zaidi karibu tuwasiliane. Lakini pia mbinu hii haimfai kila mtu. Kama umeajiriwa ni vigumu sana kutumia mbinu hii, hata kama muda huo unatumia kufanya kazi za mwajiri wako, kuna kelele nyingi kwenye ajira, vikao, ripoti na mengine.
Pia kama unafanya biashara ambayo inakutegemea wewe moja kwa moja, au wateja wanakutegemea wewe muda wote, mbinu hii haikufai.
Nina wateja wanaonitegemea muda mwingi, lakini pia wapo wa kunisaidia kwa muda fulani. Na muhimu zaidi, kama jambo haliwezi kusubiri mpaka saa sita mchana, basi limeshanikosa.

Niwatakie wote siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.