Mauzo ndiyo moyo wa biashara yoyote ile, kwa kuwa mzunguko wa fedha ni damu ya biashara, hivyo kinachosukuma mzunguko wa fedha ni mauzo, kama moyo unavyosukuma damu. Hii ina maana kwamba, kama biashara haiuzi, basi biashara hiyo inaelekea kufa, na hakuna namna ya kuiokoa bila ya kuongeza mauzo.
Leo tutakwenda kujifunza na kujikumbusha njia tano za kuongeza mauzo kwenye biashara yako, ambazo unaweza kuanza kuzitumia mara moja na ukaanza kunufaika na njia hizi.
Njia ya kwanza ni kuwauzia zaidi wateja ambao unao sasa.
Sasa hivi kuna wateja ambao tayari unao kwenye biashara yako. Hawa ni wateja wazuri sana wa kuanza nao, kwa sababu mpaka wananunua kwako, tayari kuna imani ambayo wameshaijenga na wewe au na biashara yako. Jukumu lako sasa ni kujua tatizo ambalo wanalo, na ukaweza kulitatua zaidi. Jua huduma ipi wanahitaji zaidi, au bidhaa ipi wanaihitaji, kisha angalia namna gani unaweza kuwapatia bidhaa hiyo.
Kama biashara yako ipo kwenye wakati mgumu kimauzo, angalia yale mahitaji ya msingi ambayo kila mtu anayahitaji kwa wakati huo, na kazana kuwapatia wateja wako mahitaji hayo zaidi. Njia hii itakuwezesha kuongeza mauzo na kuifanya biashara iendelee kuwa hai.
SOMA; Cross-Selling Na Up-Selling, Mbinu Mbili Za Kuongeza Mauzo Bila Kuongeza Wateja.
Njia ya pili ni kuwarudisha wateja wa zamani.
Wapo wateja ambao walikuwa kwenye biashara yako lakini siku hizi umekuwa huwaoni. Huenda wamepata sehemu nyingine wanayopata huduma kama zako, au wamekwenda mbali zaidi au wamejisahau tu, hawajasikia kutoka kwako siku nyingi. Angalia njia unayoweza kuwaikia wateja hawa, kama ulikuwa umetunza mawasiliano yao, wasiliana nao kuwakaribisha kwenye biashara yako tena. Waandalie zawadi au ofa maalumu kwa kurudi kwenye biashara yako na hapo wape huduma nzuri ili muendelee kuwa pamoja.
Njia ya tatu ni kuwaomba wateja wa sasa kuwaambia watu wao wa karibu.
Ipo njia moja rahisi sana ya kutangaza biashara, isiyo na gharama na yenye kuaminika kwa silimia 100. Njia hii ni mtu kumwambia mwenzake kuhusu huduma au bidhaa aliyopata. Pale watu wanaoaminiana wanapoambiana kuhusu biashara, wanaamini zaidi kuliko kusikia tu kwenye matangazo. Hivyo tumia nafasi hii kuwaomba wateja wako wa sasa, kuwaambia watu wao wa karibu ili nao waje kwenye biashara yako na kunufaika. Waombe kama wanawajua watu wenye shida kama wanazopata suluhisho kwenye biashara yako, wawape taarifa ili nao waweze kuja. Unaweza kuweka zawadi au ofa kwa wale ambao wanawaleta watu kwenye biashara yako. Hapo utaongeza wateja na mauzo zaidi.
Njia ya nne ni kuuza bidhaa zinazoendana pamoja.
Angalia bidhaa au huduma zote ambazo unatoa, kisha angalia zipi ambazo unaweza kuziuza kwa pamoja. Mteja anaponunua bidhaa moja, mwoneshe na bidhaa inayoendana na hiyo, na unaweza kumwuzia zote kwa pamoja. Hii ni njia nzuri ya kuongeza mauzo, ambapo mtu akinunua kitu kimoja, anaondoka na kitu kingine. Njia nzuri ya kufanya hivi ni kuuza bidhaa ambayo ni muhimu, lakini bei yake ni ya chini zaidi ya kile ambacho mteja amenunua. Kwa mfano kama unauza kompyuta, na mteja amenunua kompyuta ya shilingi milioni moja, ni rahisi kumuuzia begi la elfu 50, na flash ya elfu 10. Kwa kumwambia mteja kuhusu bidhaa nyingine anazoweza kununua, unaweza kuongeza mauzo zaidi.
SOMA; Mbinu Kumi Anazoweza Kutumia Mfanyabiashara Mchanga Kuongeza Mauzo.
Njia ya tano ni kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii.
Sasa hivi karibu kila mtu ambaye ni mteja wako anatumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Hivyo unaweza kutumia njia hizi kuongeza mauzo ya biashara yako zaidi. Unaweza kuwapa wateja wako taarifa kupitia mitandao hii. Unaweza kuwasiliana nao kwa mitandao hii na pia unaweza kutoa zawadi au ofa mbalimbali kupitia mitandao hii. Uzuri wa mitandao hii, hasa ya kijamii kama facebok, unaweza kuchagua taarifa zako ziwafikie watu wa aina gani na waliopo wapi. Kwa mfano kama biashara yako ipo sumbawanga, unaweza kuweka tangazo kwenye facebook ambalo litawafikia watu wa sumbawanga tu. Gharama yake inakuwa ndogo na linawafikia wengi na wanaohusika. Unahitaji pia kuwa na blog inayotoa maelezo kuhusu biashara yako, ambapo watu wanaotafuta suluhisho la matatizo yao kwenye mtandao wa intaneti, wanaweza kukufikia kupitia blog yako.
Hizo ndiyo njia tano za kuongeza mauzo ya biashara yako ambazo unaweza kuanza kuzitumia mara moja. Anza sasa kuzifanyia kazi kulingana na biashara unayofanya. Na kama unahitaji msaada wangu wa moja kwa moja wa jinsi ya kutumia njia yoyote kati ya hizo kwenye biashara yako, tuwasiliane kwa simu 0717396253. Karibu sana tufanye kazi pamoja ili kuweza kuongeza mauzo kwenye biashara yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog
Njia Tano (05) Za Kuongeza Mauzo Kwenye Biashara Yako Unazoweza Kuanza Kuzitumia Mara Moja Na Kufaidika.